Wilaya ya Mafia ina watu wachoyo na wabinafsi kuliko maeneo mengine

Salama mkuu, Habari za Majukumu zaidi. 🤝

1. Kuhusu usalama kwa kweli pako vizuri, Kambi ya Jeshi ipo huku kuna sehemu inaitwa MLALI, pia kuna magereza kwa wale wenye makosa kadhaa, kituo cha police kimoja pamoja na askari mgambo kwenye vijiji vya pembeni.
(a) usafiri upo wa Aina mbili, majini na angani hivyo endapo utasafiri utalazimika kuwa na vitambulisho vinavyo tambulika na JMT.

(b) Usafiri wa MV KILINDONI ambayo ni pantoni, ambapo upande wa bara utapandia NYAMISATI na upande wa kisiwani utapandia KILINDONI- kigamboni,

(c) ingawa kuna baadhi ya njia za panya kutoka kigamboni mpaka kisiwani mafia - Bweni, hii ni njia ya kusafirishia samaki pekeki kwa kutumia majahazi lakini wamekuwa wakikiuka sheria ndogo ndogo za usafiri wa majini hivyo kupakia na abiria.

(d) njia ya panya nyingine ni kutoka bara nyamisati kupitia njia ya bwa juuu( bwa juu ni kisiwa kisicho kuwa na baiskeli, pikipiki wala gari 😋😋 ) kuelekea kilindoni, hapa pia watu hupanda usafiri wa hatari zaidi maana njia hii siyo salama hasa mawimbi yakiwa makubwa maana kuna makutano ya mto rufiji pamoja na bahari ya hindi.

( e) pia unaweza kufika visiwa vya comoro kutoka mafia kupitia bahari kuu zinakopita meli kubwa za mizigo, hivyo safari hii huchukua takribani wiki tatu hadi nne.

ii) maisha ya noti ipo hasa upande wa mali mbichi na Usafirishaji wa nazi kutoka mafia hadi dar es salaam kupitia kibiti, mkulanga.
 
Point No 2 imenishangaza
 
Ahsante panapo majaliwa nitakuja .
 
Huku kupewa kesi ni nje nje, yani mda wote wanatamani mtumishi atimuliwe kazi.. 😁
 
Nakubaliana nawe mleta mada , ni sehemu iliyo duni kifikra, kimtazamo kiakili na hata utashi.
Hadi nuru ya maendeleo ya ujumla wake iwaangazie kutakuwa kumekuchwa sana, ni moja wapo ya sehemu ya hivyo ingawa kwa wenyeji ni pa thamani sana.
Huku ni changamoto sana, hii wilaya ingekuwa ina watu wenye roho zuri hakika ingekuwa mbali sana kimaendeleo.
 
Is why maendeleo huko. Ni very low. Mindset ya jamii husika ndio chanzo kikuu. Aina hiyo ya watu ni vigum kupiga hatua, wanaupenda umasikini sana
Haya ni matangopori ambayo mnalishana Humu, mikoa yote ya Pwani Gdp per capita ipo juu kasoro tu mkoa wa Pwani,

Tanga, Dar, Lindi, Mtwara etc zote zipo juu

Hii ndio mikoa masikini yenye maendeleo madogo nchi hii

1.Simiyu =1.54
2.Kagera =1.58
3.Singida =1.64
4.Pwani =1.81
5.Dodoma =1.89
6.Tabora =1.95
7.Kigoma =2.0
8.Katavi =2.1
9.Songwe =2.4
10.Rukwa =2.5

So kama unataka watu wa kuwananga watafute hao.

Lindi na mtwara si mikoa masikini isio na maendeleo, wanapiga hela nyingi tu huko kwenye korosho, uvuvi etc.

Source NBS kupitia hapa
 
Ukienda na hizo chuki ulizojaza ni lazima utapata taabu mahali popote. Vingi ulivyoandika ni uongo mtupu. Safisha roho utaona watu wanakupokea popote. Usiende mahali ukajiona wewe mfanyakazi serikalini ni daraja la juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…