Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
WILAYA YA MUSOMA - FURSA ZA KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO
Tarehe ya Kongamano: Jumatatu, 30 Dec 2024
Mahali: Kiwanja cha Mukendo, Manispaa ya Musoma
Mgemi Rasmi: Mhe Juma Issa Chikoka, Mkuu wa Wilaya, Wilaya ya Musoma
Mchango wa Prof Sospeter Muhongo, Mbunge, Jimbo la Musoma Vijijini
Mbunge ameainisha maeneo ya uwekezaji yatakayokuza uchumi wa Wilaya ya Musoma, kwa haraka (8-10% growth), na kuongeza kwa kasi ya upatikanaji wa ajira mpya na maisha bora zaidi.
Maeneo makuu ya uwekazaji:
(i) Elimu bora na Elimu ya ufundi
(ii) Uvuvi: vizimba na viwanda vya samaki
(iii) Kilimo cha umwagiliaji na viwanda vya usindikaji mazao, na kiwanda kipya cha nguo
(iv) Ufugaji: maziwa na kiwanda cha maziwa, n.k.
(v) Uchimbaji madini: dhahabu, gesi ya helium, n.k.
(vi) Utalii: visiwa ndani ya Wilaya yetu, n.k.
VIDEO/CLIP iliyoambatanishwa hapa: tafadhali sikiliza sehemu ya mchango wa Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 30 Dec 2024