A
Anonymous
Guest
Wilaya ya Mvomero haijishugulishi na mji wake
Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro ni kama haipo.
Wilaya hii eneo lake la centre (uso wa mji wa Mvomero) ni eneo moja linaitwa Wami Dakawa dakika 05 kwa gari toka Wilaya ilipo hadi hapa ilipo centre yake Wami Dakawa.
Eneo hili limekuwa makazi ya mafuriko mwaka hadi mwaka, hii itadhibitishwa na mtu yoyote anayepita eneo hili kwa kutumia barabara ya Morogoro-Dodoma wakati Mvua.
Mafuriko yakitokeo ndio utamuona Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wakifika na waandishi wa habari kutoa pole, kisha hupanda magari na kuondoka.
Aidha, chanzo cha mafuriko katika eneo hili moja ni ukosefu wa mitaro katika eneo la Wami Dakawa hasa pembezon mwa barabara kuu ya Morogoro Dodoma
Pili ni kutokana na kujaa kwa udongo katika mtaro mkubwa unaozunguka eneo la wami Dakawa. Mtaro huo ulichimbwa mwaka 1976 tokeo hapo haujawahi kufanyiwa marekebisho na hivyo kujaa tope na maji yanapokuja yanakosa sehemu ya kupita na kusambaa katika makazi ya watu.
Aidha, wananchi wa mtaa wa funga funga (Dakawa) waliamua kujichangisha fedha na kuchimba nusu ya huu mtaro kuanzia barabara inayoelekea kiwanda cha sukari Mkulazi hadi barabara ya idara ya maji Nelemko, nusu ya mtaro haijaguswa hivyo mvua ikinyesha kero ya mafuriko bado ipo pale pale.
Ushauri Kwa wilaya
Wami Dakawa ndio mji pekee uliopo katika uso wa Ofisi za Wilaya Mvomero, je mapato ya Wilaya hii yanafanya kazi gani?
Nashauri:
1. Kuchimbwa na kuboreshwa kwa mitaro iliyopo wami Dakawa hasa pembeni ya barabara ya Moro -Dodoma
2. Kuchimbwe na kufukuliwa kwa mtaro mkuu unaozunguka mji wa Dakawa upande wa Magharibi ili kuzuia maji kusambaa katika makazi ya watu
2. Kufanyike upanuzi wa parking za Malori ili malori yapate sehemu za kupark na kuchangia uchumi wa eneo hili na mapato ya Serikali, lakini pia kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara sababu ya ufinyu wa parking za maloari na magari yanayopita.
3. Kuwekwa taa za barabarani ili kuleta mvuto wa mji na kuongeza mwanga wakati wa usiku.
Pichani ni wakati wa mafuriko na mtaro uliochimbwa na wananchi wenyewe