Siku chache zilizopita nilikuwa katika moja ya vijiji vinavyounda Wilaya mpya ya Rorya-zamani Tarime.
OCHUNA KIJIJI CHA UJAMAA
Kijiij cha Ochuna kipo Kata ya Nyathorogo,Tarafa ya Luo-Imbo Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.
Kijiji hiki kina wakazi mchanganyiko wa makabila mawili (a) Wajaluo (b) Wakurya/wasimbiti-Rieny.
Kwa upande wa Mashariki Ochuna inapakana na Wilaya ya Tarime-Vijiji vya Bukenye/Komaswa,
Kwa upande wa Kusini inapakana na Tingirime/Kisumwa. Kaskazini ni Kowaki na kwa upande wa Magharibi inapakana na vijiji vya Kamot-Chereche,det,Obolo na Mlima Rorya ambao ndio mrefu kuliko yote yumkini katika Wilaya ya Rorya na Tarime kwa ujumla.
Kijiji hiki ni maarufu kwa kilimo cha Mpunga,Mtama na Mahindi.Kwa siku za hivi karibuni Mpunga ndilo zao kuu la biashara,pia ni wafugaji japo siku hizi hakuna wenye idadi kubwa ya mifugo kama ilivyo kuwa zamani-nafikiri ni kutokana na wimbi kubwa la wizi wa mifugo.
Kama ilivyo kwa vijiji vingine vya Mkoa wa Mara,umaskini umetamalaki kwa kiwango cha kutisha,naweza diriki kusema kuwa Ochuna ni kijiji kilichotelekezwa kwani hakuna uongozi wowote unaotambulika/wajibika kwa wananchi na hata wageni wanaofika Ochuna! (Hakuna Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji wala Afisa Mtendaji wa Kijiji kwa zaidi ya miaka miwili).
Yupo Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji anayekaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Kiongozi huyu inasemekana amekwisha maliza muda wake wa kutumika ila ameombwa kusaidia shughuli za serikali (Usiniulize hadi lini na analipwa bei gani kwa Msaada anaoutoa)
Ndugu zangu sio lengo langu kuelezea hali tete ya kiuongozi inayokabili kijiji hiki,bali ni kueleza Hatari niliyosimuliwa na kushuhudia kwa macho yangu kwa takriban wiki moja niliyokaa Ochuna.
UFUSKA,Umalaya uliyo kubuhu
Katika msimu huu wa mavuno kumeibuka aina fulani ya Muziki unaochezwa nyakati za usiku (Disko vumbi).
Kama kuna eneo HATARI kwa afya ya vijana wenzangu na ustawi wa Rorya na taifa kwa ujumla ni suala zima la huu muziki wa usiku unaopigwa popote penye mkusanyiko wa watu au penye uwezekano wa watu kukusanyika kwa wepesi hasa nyakati za usiku.
Kwa kawaida hakuna mwaliko rasmi wa kuucheza muziki huu na wala hakuna kiingilio chochote kinachotozwa ili kuhudhuria muziki huu. Vijana wanafuatisha sauti ya muziki na mara moja hujua kuwa leo muziki upo mahali fulani au kwa mji fulani.
Mara nyingi hutegemea Siku ya soko/mnada/chiro na penye MSIBA (siku chache baada ya mazishi)
Nilipofika kijijini kushiriki msiba wa ndugu yangu aliyefariki 18/06/2013 mara baada ya mazishi alikuja ndugu yetu mmoja akatukuta pamoja na kaka yangu tuliesafiri nae toka Dar-Es-Salaam kwenda kwenye huo msiba ilikuwa Jumatatu 24/06/2013 ghafla akaanzisha mada juu ya huo muziki na wasichana -Maids wenye uwezo mkubwa wa kucheza na kurejesha fedha/gharama iliyotumika kuwaleta na faida zaidi ya mara nne! Hakika tulivutiwa kwani kama ujuavyo Msiba ni msiba pesa zinatumika sana,basi kaka yangu tuliesafiri nae toka Dar-Es-Salaam akaamua kutoa kiasi cha Shilingi Elfu 30 Tshs. Gharama za kukodi muziki tukaambiwa hizo ndizo gharama za kuleta muziki na wacheza shoo.
Muda ulipofika kweli muziki uliletwa na watu wakajaa.
SIKITIKO LANGU
Nikiri mapema kuwa mimi ni mzaliwa wa Ochuna na utamaduni huu wa kuleta muziki baada ya mazishi ya mpendwa wenu upo miongoni mwetu sisi wajaluo,japo hali hii nimezaliwa nimeikuta lakini hakuna mahali nilishuhudia au hata kusimuliwa juu ya uchafu huu nilioshuhudia kipindi hiki -Wasichana kuvua nguo zote na kucheza Uchi huku vijana ambao wengi wao ni wa umri wa kati ya miaka 14-25 wakicheza nao wao pia wakiwa na Pombe za kwenye mifuko ya Plastiki Mfano Vodka,burudani,konyagi n.k wametia mifukoni mwao na hutoa pakiti moja baada ya nyingine na kunywa huku wakiendelea kucheza.
Baada ya muda mfupi wote wasichana kwa wanaume(tamka vijana wadogo) wanakuwa hawajitambui kwa ulevi na kufanya ngono bila hata ya tahadhari/kinga yoyote!
Ukweli ni kwamba Msichana anae vua nguo mbele ya wanaume tena bila woga/kificho amejiandaa kwa jambo moja tu-NGONO.
Hofu yangu inatokana na ukweli kuwa mara zote wasichana wanaocheza namna hii hawatoki ndani ya kijiji husika,mara zote hutolewa kijiji/vijiji vya jirani! Sasa,kwa mzunguko huu tutarajie nini kwa wadogo zetu ambao wengi wao ndio kwanza wako kidato cha pili au tatu?
Kwa mzunguko huu tafsiri yake ni kwamba Muziki ukiwa Buturi watachukuliwa wasichana toka Ochuna,Kowaki,Kamot au Utegi na muziki ukiwa Utegi wasichana watachukuliwa toka Mara-Sibora,Komaswa au Buturi!
Kuna kufaulu masomo kweli? Na vipi afya zao baada ya miaka 5 ijayo? Kumbuka Madhara ya Pombe kali na hasa hizi pombe kali zinazofungwa kwenye pakiti za plastiki na kuuzwa kwa bei rahisi (Mobile Alcohol) unaweza kuibeba na kwenda nayo popote! Vipi matumizi ya kinga wakati wa ngono?
Nijuavyo mimi,akili iliyojaa pombe haiwezi fikiria matumizi ya kinga wakati wa ngono.
Nihitimishe kwa kusema kwamba,umefika wakati tubadili mienendo yetu,sio muda wa kuitupia lawama Serikali au mtu awae yote,tujisaidie sisi wenyewe ili wale ndugu zetu pia wapate kujifunza toka kwetu. Vinginevyo Rorya kwishaaaaaaaaaaaaa ndani ya miaka 10 tu ijayo. TUWE NA HOFU YA MUNGU
Nitafute kupitia : wycliffe181@gmail.com