Pre GE2025 Wilfred Lwakatare afichua sababu za kutojiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Uenyekiti CUF

Pre GE2025 Wilfred Lwakatare afichua sababu za kutojiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Uenyekiti CUF

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
“Endapo nikikuta jina la Profesa Ibrahim Lipumba katika karatasi za wagombea uenyekiti najitoa.” Hii ilikuwa kauli ya aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatare.

Licha ya kutoa kauli hiyo mara mbili kwa nyakati tofauti alipozungumza na Mwananchi, Lwakatare ameshindwa kuisimamia baada ya jana Jumatano, Desemba 18, 2024 kushiriki uchaguzi kuwania uenyekiti akichuana na Profesa Lipumba.

Mara ya kwanza Lwakatare alisema: “Nikikuta kuna fomu ya Profesa (Lipumba), mimi ya kwangu naiondoa… kwa sababu namheshimu sana na ameshanitamkia mara tatu kwamba hagombei, sasa tutakwendaje namna hiyo kwa kuviziana.”

Hata hivyo, Lwakatare ambaye ni mbunge wa zamani wa Bukoba Mjini ameliambia Mwananchi leo Alhamisi, Desemba 19, 2024 kuwa aliamua kutojitoa katika kinyanga’nyiro hicho baada ya wajumbe wanaomuunga mkono kumshawishi.

Katika uchaguzi ambao matokeo yalitangazwa usiku wa kuamkia leo, Lwakatare alishindwa kufua dafu mbele ya Profesa Lipumba aliyepata kura 216 kati ya kura 592 halali zilizopigwa. Lwakatare alipata kura 78.

Lwakatare CUF.png


Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom