Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
Gidabuday amefariki akiwa na miaka 50, siku chache kabla ya kumkumbu ya siku yake ya kuzaliwa 19/09/1974, akiwa ni mtoto wa kwanza wa mzee Francis Gidabuday, akiwaacha wadogo zake wawili wa kiume na mmoja wa kike.
Gidabuday, amemuacha mke na mtoto mmoja wa pekeevwa kiume (ambaye ni raia wa marekani Sydney Gidabuday ) mwanae anaishi Colorado huko marekani ambako ndiko alikozaliwa , japo hatoweza kufika kwenye mazishi ila familia itaendelea na maziko. Gidabuday alimzaa Sydney wakati akiwa marekani kimichezo na elimu ya chuo, na baadae kurudi Tanzania na kuendeleza riadha hadi kufikia cheo cha ukatibu mkuu wa shirikisho la riadha tanzania.
Gidabuday ameacha alama kwenye riadha hasa kuzungumza bila kuogopa na kuwezesha kuleta baadhi ya wawekezaji kwenye mchezo wa riadha.
Gidbuday, ameacha taasisi yake inayoshugulika na riadha na utalii.
Pia soma: Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha, Wilhelm Gidabuday afariki dunia kwa kugongwa na gari