Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wenyeviti wa mitaa, vijiji, vitongoji na wajumbe wa halmashauri ya kijiji kundi maalumu wanawake na mchanganyiko wameapishwa katika kata tofauti tofauti za wilaya ya Makete mkoani Njombe
Uapisho huo umefanyika leo Novemba 28, 2024 na kuongozwa na Hakimu Mkazi Denis Rwelamiba Mjwahuzi siku moja tangu kumalizika uchaguzi wa serikali za mitaa uliowaweka madarakani viongozi hao
Akiwa katika zoezi la kuwaapisha viongozi waliochaguliwa katika kata ya Tandala, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete, William Makufwe ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri hiyo amewapongeza kwa kuaminiwa na wananchi huku akiwasihi kwenda kutenda haki katika kutekeleza majukumu yao
Sanjari na hilo amewasisitiza kufuata sheria kanuni na taratibu huku pia wakitumia hekima na busara katika kufanya kazi.