Wilshere huyu tutakuwa nae Russia endapo kama hatokwenda kupumzika hospital katika roundi hii ya pili ya EPL

Dkileo

Member
Joined
May 23, 2017
Posts
51
Reaction score
46
Wilshere huyu tutakuwa nae Russia endapo kama hatokwenda kupumzika hospital katika roundi hii ya pili ya EPL

Nimejaribu kumwangalia kwa umakini mkubwa sana Jack Wilshere katika mechi nne za Epl za Arsenal zilizopita..Dhidi ya Westham,Newcastle,Liverpool na Crystal palace..Bado Jack anauwezo wa kuonyesha ubora Zaidi..

Katika game dhidi ya Livepool kiungo cha Arsenal kilikuwa vibaya sana..Haswa kipindi cha kwanza..Lakini kipindi cha pili Arsenal walirudi imara na nilianza kumwona Wilshere akikatiza mbele ya viungo wa Liverpool Emre Can na James ilner.Na hata alipoingia wijnaldum bado Wilshere pamoja na Xhaka waliweza kuwamiliki viungo watatu wa Liverpool

Jack huwa ana jiamini mno..Ni kipaji maridhawa sana.Nni kiungo ambaye haogopi kutembea na mpira..Ni kiungo anaye weza kukupiga chenga na kuondoka zake…

Naaangalia viungo hawa wa kiingereza (Milner,Henderson,Jack Livermore na wengineo) bado naona nafasi ya Wilshere katika kikosi cha England 2018 world cup Russia....Hasa katika kipindi hiki ambacho England haina vipaji vingi katika timu zao kubwa…England katika kiungo haina frank Lampard,Paul Scholes,Steven Gerrard wala Michael Carrick..

Katika kipindi hiki ambacho Aaron Ramsey anaumwa bado naona Wilshere anavyo zidi kupata nafasi katika kikosi cha Arsenal..Viungo anaobaki katika benchi la Arsenal ni defensive minded (Elneny na Coquelin ) na ningumu kwa Wenger kuanza na viungo wakabaji wawili haswa anapokuwa anatumia mfumo wa mabeki watatu wa kati..

Endapo kama hato pata majeraha ya kumweka nje kwa muda mrefu basi Wilshere tutakuwa nae Russia 2018..Mark my words
 
Binafsi namkubali sana uyu kiungo, Mungu amsimamie
 
Ramsey aendelee kuwa mgonjwa tu maana mr bean anampenda ili Jack atupe mambo
 
Katika wachezaji wote wa kiingereza huyu jamaa ndio anaujua mpira haswa, trust me lau kama angekuwa hana majeruhi ya mara kwa mara basi angekuwa yuko mbali mnoo, dunia ingekuwa inamzungumzia moja kati ya viungo bora wa zama hizi
 
Umenikuna sana, sio kwakuwa mimi ni mdhamini wa Gunners la hasha. Namkubali sana Will Power!!
 
Jack yupo vzur sana... ni kiungo ambaye huwa nataman kumtazama kila anapogusa mpira
 
Huyo dogo majeruhi tu ndio yanataka kuharibu carrier yake, nakumbuka kwenye game ya Arsenal vs Barcelona pale emirate, barca anakufa 2-1 jack alifanya xavi na sergio waonekane wa kawaida sana

Baada ya game pep alisema kama jack majeruhi yatampita kushoto basi ni miongoni mwa viungo wazuri kuwahi kutokea England
 
Huyo ndio Jack anajua kudrible , ananyambulika

Namuelewa sana jack

Mungu amuepushe na majeraha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…