Wimbi la kampuni za kitanzania za kuagiza magari; uaminifu na uhalisia

Wimbi la kampuni za kitanzania za kuagiza magari; uaminifu na uhalisia

Mtanzanyika

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2015
Posts
368
Reaction score
425
Habari wakuu,

Miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi la kampuni za kitanzania zinazoagiza magari kutoka Japan, UK, Singapore n.k. Tena wana utaratibu wao wa malipo kwa awamu mbili, unalipa unapoagiza gari na malipo ya pili unamalizia gari linapofika. Kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Instagram nadhani mtakuwa mnakutana sana na post za hayo makampuni, yapo mengi sana. Sasa ningependa tupeane elimu hapa kuhusu hayo makampuni:-

(1) Je hakuna harufu ya utapeli.?
(2) Kwa nini yote yana utaratibu unaofanana wa malipo kwa awamu mbili.?
(3) Je wao huko Japan hayo magari wanayanunua kutoka wapi.?

Karibuni kwa mawazo na ushauri na kama kuna nyongeza ya maswali mengine ya ufahamu kuelimishana zaidi.
 
Mimi naona labda aje mtu ambaye ameshawai kuagiza na haya makampuni ila kwangu mimi naona kama ni MAENDELEO, kinachotakiwa haya makampuni yafanye kazi kwa kuzingatia :-

1. Uaminifu
2. Unataka
3. Ubora wa magari
4. Watoe ushauri mzuri kwa wateja na wasiwe wajanja wajanja
 
Ukifanya research kidogo hapa JF na kwenye internet kwa ujumla unaweza kuagiza gari peke yako bila kutumia hizo kampuni za pembeni kwenye process ya kuagiza. Mwishoni ukachagua kampuni ya clearing and forwarding (ambazo unaweza watumia hao hao uliponunua gari kwao) wakakusalia process ya kulipa ushuru na kulitoa bandarini. Mwisho wa siku utalipa kwa awamu mbili pia, na gharama itapungia pia.
 
Biashara imebadilika Tanzania baada ya makampuni mengi ya kuuza Magari kuwa ngumu ndio maana wamekuja na biashara ya kuagiza Tu basi.

Leo hii ulete Magari 40 alafu uyauze Kwenye yard itachukua mwaka mzima hayajaisha,sio kweli kwamba makampuni mengi ni matapeli
 
Tatizo lao ni kutokuwa waaminifu kwa hawa wanaouza magari ndiyo maana yanachukua muda mrefu kwenye yard zao.

Gari, wanavyolitoa Japan sivyo utakavyolikuta likishafika Bongo. Utakuta wameshabadilisha vitu wameweka yakwao. Ndiyo maana watu wanaamua kuagiza wenyewe.
 
Wabongo Kwenye biashara tunazingua Sana kwa hapa dar kuna yard ni waaminifu Sana na zipo yard wanachakachua mpaka milage ya gari unakuta hiyo gari imetembea km 190000 lakini wanachokifanya kurudisha Hadi km 60000.

Yard zenye akili hapa dar zipo Kinondoni manyanya,namanga msasani na victoria
 
Back
Top Bottom