Watu tumeshadata
Na hili ghetto life style
Shad bakren au nelly wa x-plasta
Hey dark master nitembezee chata
Kisha nipe kipaza nihubiri kama pastor
Ndani ya ghetto ni mengi yashatukuta
Lakini masela bado tunakomaa kutafuta
Bado tunazisaka hata kwenye vichaka
Atafutae hachoki akichoka ndio ameshapata
Japo sometimes kile kitu unachopata ni tofauti kabisa na kile unachotaka
Ila mwanaume lazima ujifunze kuridhika kwani ukichagua sana hukawii kutoka kapa
Duniani wote hatuwezi kuwa sawa na ndio maana wapinzani wa jadi mnapagawa Kama nipo juu ni juu
Ningoje chini, au nifate juu uvunjike guu
Masuper star tunang'aa kwa pamba tunazovaa
Zinaficha njaa, ila tunapokaa
Wengine nyumba ta udongo nyasi mlango wa gunia
Ndani hakuna mwiko kikombe wa sufuria
Zaidi ya kiberiti tu na kipande cha mkeka
Na nikishakula mambo yangu nauweka
Wala sioni hatari kula dona dagaa
Si kuna wengine hawajauona wamelala na njaa
Na usione tumepinda migongo, ukadhani ni vibyongo
Pengine ni ufupi tu wa mlango
We endelea kula bia acha mi nikapate gongo
Mradi wote tuwe stim ndio life ya kibongo