Wimbi la ndugu wa damu kuhusiana kimapenzi linaongezeka au uwazi umeongezeka?

Wimbi la ndugu wa damu kuhusiana kimapenzi linaongezeka au uwazi umeongezeka?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa mzazi inaweza isikuingie akilini kwamba watoto wako unaoishi nao nyumba moja wanaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi, ila ukweli uko hivyo, yapo matukio mengi ya aina hiyo ambayo yanaendelea kushika kasi kwenye jamii.

Hii inahusisha ndugu wa damu, ndugu wa familia au ukoo na hata baba na mtoto ambayo kwa tamaduni zetu wanaitwa maharimu.

Kwa sheria za Tanzania, ni kosa maharimu kujamiiana au kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini huenda utandawazi umefanya jambo hili kuanza kuonekana kawaida na matukio ya ndugu kuwa na uhusiano wa kimapenzi yameanza kuingia kwenye jamii yetu.

Mfano wa hili ni kile kilichotokea Agosti 14, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ilitoa hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela kwa Mussa Shija (32) na miaka 30 jela kwa Hollo Shija baada ya kukutwa na kosa la kujamiiana na maharimu.

Mahakama ilithibitisha wawili hawa kuwa ni ndugu wa damu waliokuwa na uhusiano wa kimapenzi, wakiishi pamoja kama mume na mke kwa zaidi ya miaka mitano na kufanikiwa kupata mtoto mmoja.

Kesi hii iliibua mjadala kwa wengi, wakihoji inawezekanaje kwa ndugu wa damu kuwa na uhusiano wa kimapenzi hadi kufikia hatua ya kuishi pamoja kama mke na mume?

MWANANCHI
 
Jirani yetu ana watoto wawili, wa kiume (11) wa kike (5)
Mtoto wa kike akamwambia jirani mwingine kua kaka yake anam'baka.

Mama mtu alipoambiwa alimchapa yule mtoto wa kike, eti kwanini kawaambia majirani.
Na hapa ndio chanzo cha tatizo, wazazi kufanya swala la mtoto kuingiliwa kuwa ni fedheha.
 
Mabinti kuvaa nguo zisizo na stara,,,mapaja njee mbele ya kaka zao....wanajidanganya et kwa ndugu hisia hazipandi
 
Back
Top Bottom