SoC04 Wimbi la ugonjwa wa shinikizo la juu la damu (pressure/ hypertension) na madhara yake vinaweza kudhibitiwa mapema kuanzia ujanani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Copro mtego

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
619
Reaction score
796
UTANGULIZI
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu umekuwa ugonjwa unaoongoza kuathiri watu miongoni mwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa. Kwa takwimu za mwaka 2024 zilizotolewa na Journal of Human Hypertension zinaonesha kuwa 48% ya watu wote kusini mwa jangwa la Sahara wana ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Ugonjwa huu unazidi kukua kwa Kasi miongoni mwa watanzania na madhara yanayotokana na huu ugonjwa yanajitokeza kila muda katika nchi yetu.

Watu ambao wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa wa shinikizo la juu la damu kwa siku za hivi karibuni ni vijana wenye kipato cha chini na kati tofauti na ilivyokuwa kwa siku za nyuma ambapo watu wenye kipato cha juu na wenye umri mkubwa ndio walio athirika zaidi na ugonjwa huu.

Mitindo ya maisha wanayoishi vijana inayoongeza hatari ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Matumizi makubwa ya chumvi mbichi

Matumizi ya chumvi mbichi linawafanya watu wawe kwenye harari kubwa ya kupata ugonjwa huu. Chumvi mbichi imekuwa ikitumika zaidi kwenye supu, vyakula vya kuchoma mfano nyama choma, vyakula vya kukaanga kama vile mihogo, chips,popcorn na clips. Vyakula hivi umekuwa vikiliwa kwa wingi hivyo kusababisha ongezeko la matumizi ya chumvi mbichi na kuhatarisha ongezeko ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Vijana wengi hasa wenye kipato cha chini hutumia mihogo kama chai ya asubuhi.

Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
Hii ni kwa sababu sukari ikiwa nyingi mwilini hubadilishwa na mafuta hivyo kupelekea mafuta kujipanza kwenye Kuta za mishipa ya damu na kupelekea ukinzani kwenye mishipa ya damu kuongezeka (peripheral resistance) Kisha kusababisha shinikizo la juu la damu. Kumekuwepo na ongezeko la ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi mfano ice cream, keki, soda, na vinywaji vingi vya kusindikwa.

Ongezeko la kazi za kukaa na zisizotumia nguvu.
Tofauti na siku za nyuma, vijana wengi wa sasa hawafanyi shughuli za kutumia nguvu sana. Vijana wengi wanajihusisha na kazi kama ya boda boda , udalali, biashara ndogo ndogo,na kazi za ofisini. Kundi kubwa la vijana wanajihusisha na shuhjuli hizi ni vijana hivyo huwapelekea muda mwingi wasiwe wanatumia nguvu na kuwasababishia wasifanye mazoezi kupitia shughuli zao.

Matumizi ya pombe kali na sigara.
Vijana wengi wanatumia vileo vikali ambavyo hupatikana kwa huuzwa kwa bei ya chini. Pombe hizi zimekuwa zikitumiwa na vijana wa kipato cha chini kwa sababu ya gharama yake kuwa chini . Pia sigara zinatumiwa sana na vijana wengi na pia huwaathiri na watu ambao wanaishi nao. Uvutaji wa sigara unaongeza hatari kupata ugonjwa wa shinikizo la juu la kwa zaidi ya mara kumi.

Madhara ya shinikizo la juu la damu
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu hauna dalili za moja kwa moja hadi madhara yake yanapojitokeza baada ya muda mrefu. Ugonjwa huu usipogundulika mapema na kuanza tiba yake unaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya hata kifo cha ghafla.

Madhara ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ni kiharusi (stroke),matatizo ya moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebrovascular accident), figo kushindwa kufanya kazi (chronic kidney failure), kuharibika kwa mishipa mikubwa ya damu (aortic aneurysm) na mengine mengi.

Baadhi ya mitindo ya maisha ambayo inaweza kuondoa vijana kwenye hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ni kama ifuatavyo

Kupunguza matumizi ya chumvi
Kwa kuwa chumvi nyingi (hasa chumvi mbichi) ni kisababishi cha ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, tunaweza kupunguza hatari ya ugonjwa huu kwa kuweka sera ya kuhamasisha kitotumia chumvi mbichi. Mfano sio lazima kuongeza chumvi kila ukiangiza supu hotelin au viazi vya kukaanga (chips). Vile vile hakuna ulazima wa kuchovya kwenye chumvi unapokuwa unakula nyama choma au mihogo. Kama vijana wengi wataacha kutumia chumvi mbichi kwa namna hii hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Kupunguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi
Inawezekana kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama soda na vinywaji vingine vya kusindikwa. Ikiundwa sera ya kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi kutapunguza sana hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Mfano wizara ya afya inawezekana kuanzisha kampen ya unywaji wa maji badala ya soda na juisi, ulaji wa vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi na ulaji wa matunda halisi badala ya juisi ya matunda hayo itamsaidia sana kupunguza kiwango cha sukari kinacholiwa na watanzania kwa nyakati hizi.

Kudhibiti matumizi ya pombe na sigara
Hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu inaweza kupungua ikiwa watu watadhibiti matumizi ya pombe na sigara. Tunaweza kudhibiti matumizi haya kiwaelimisha watu kuhusu kiwango cha pombe kinachotakiwa kunywewa kwa siku. Kwa kuwa vijana wengi hasa wa kipato cha chini wanakunywa pombe kienyeji na kali za viwandani, serikali inapaswa kudhibiti uzalishaji wa bidhaa hizo. Pia sigara zisivutwe kiholela kila sehemu bali kuwepo na maeneo maalum ya kuvutia sigara badara ya kuvutia kwenye mikusanyiko kama sokoni na barabarani kiholela ili kuwalinda wasiovuta sigara.

Kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara
Watu ambao hawana muda wa kufanya mazoezi wanaweza kufundishwa kufanya mazoezi kwa kutembea au kuendesha baiskeli wakiwa wanaenda kwenye shughuli zao .Pia kuna mazoezi mepesi ambayo mtu anaweza akafanya mwenyewe akiwa chumbani kwake na watu wanaweza kufanya hivyo baada ya kufundishwa na kuhamasishwa pia.

Kuhamasisha upimaji wa afya mara kwa mara na kuanza matibabu mapema
Vijana wengi hasa wa kiume hawana tabia ya kupima hali zao za afya mara kwa mara katika jamii zetu. Iwapo vijana watakuwa na tabia ya kupima afya zao hasa shinikizo la damu, itawasaidia kujua hali zao na wale watakaogundulika wataanzishiwa matibabu ili kuepusha madhara yake.

Hitimisho
Ili tuweze kuipata Tanzania iliyo imara miaka 25 ijayo na baadae, tunahitaji vijana wenye afya njema sasa ambao watakuwa wazee wenye afya hapo baadae ambao wataendelea kuwa na mchango kwenye jamii na kutengeneza kizazi bora cha miaka mingi ijayo. Ikiwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu utadhibitiwa, magonjwa mengine yasiyokuwa ya kuambukizwa kama kisukari, tezi dume, matatizo ya uzazi na mengineyo yatakuwa yamedhibitiwa pia hivyo tutakuwa na jamii yenye afya bora.
 
Upvote 25
Matumizi makubwa ya chumvi mbichi
Matumizi ya chumvi mbichi linawafanya watu wawe kwenye harari kubwa ya kupata ugonjwa huu. Chumvi mbichi imekuwa ikitumika zaidi kwenye supu, vyakula vya kuchoma mfano nyama choma, vyakula vya kukaanga kama vile mihogo, chips,popcorn na clips. Vyakula hivi umekuwa vikiliwa kwa wingi hivyo kusababisha ongezeko la matumizi ya chumvi mbichi na kuhatarisha ongezeko ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Vijana wengi hasa wenye kipato cha chini hutumia mihogo kama chai ya asubuh
Niko na swali kiasi ndugu, chumvi mbichi ni NaCl....... je chumvi ilopikwa ni kitu gani.

Aaani chumvi ikipikwa inakuwa kitu gani?
Kupunguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi
Inawezekana kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama soda na vinywaji vingine vya kusindikwa. Ikiundwa sera ya kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi kutapunguza sana hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
Penyewe hapa tunaelewana , ahsante kwa ushauri
 
Asante ndugu
Kuhusu chumvi mbichi haina utofauti kikemikali na chumvi iliyopikwa , tofauti ni kwamba ulaji wa chumvi mbichi hupelekea upate kiwango kikubwa cha chumvi kuliko kile kinachotakiwa kwa siku hivyo NaCl inakuwa nyingi kwenye damu na kusababisha maji yabaki mengi kwenye damu (retention) kitu kinachopelekea hatari ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.
 
UTANGULIZI
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu umekuwa ugonjwa unaoongoza kuadhiri watu miongoni mwa magonjwa yasiyokuwa ya kuambukizwa. Kwa takwimu za mwaka 2024 zilizotolewa na Journal of Human Hypertension zinaonesha kuwa 48% ya watu wote kusini mwa jangwa la Sahara wana ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Ugonjwa huu unazidi kukua kwa Kasi miongoni mwa watanzania na madhara yanayotokana na huu ugonjwa yanajitokeza kila muda katika nchi yetu.

Watu ambao wapo katika hatari ya kuugua ugonjwa wa shinikizo la juu la damu kwa siku za hivi karibuni ni vijana wenye kipato cha chini na kati tofauti na ilivyokuwa kwa siku za nyuma ambapo watu wenye kipato cha juu na wenye umri mkubwa ndio walio athirika zaidi na ugonjwa huu.

Mitindo ya maisha wanayoishi
vijana inayoongeza hatari ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.

Matumizi makubwa ya chumvi mbichi

Matumizi ya chumvi mbichi linawafanya watu wawe kwenye harari kubwa ya kupata ugonjwa huu. Chumvi mbichi imekuwa ikitumika zaidi kwenye supu, vyakula vya kuchoma mfano nyama choma, vyakula vya kukaanga kama vile mihogo, chips,popcorn na clips. Vyakula hivi umekuwa vikiliwa kwa wingi hivyo kusababisha ongezeko la matumizi ya chumvi mbichi na kuhatarisha ongezeko ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Vijana wengi hasa wenye kipato cha chini hutumia mihogo kama chai ya asubuhi.

Ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
Hii ni kwa sababu sukari ikiwa nyingi mwilini hubadilishwa na mafuta hivyo kupelekea mafuta kujipanza kwenye Kuta za mishipa ya damu na kupelekea ukinzani kwenye mishipa ya damu kuongezeka (peripheral resistance) Kisha kusababisha shinikizo la juu la damu. Kumekuwepo na ongezeko la ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi mfano ice cream, keki, soda, na vinywaji vingi vya kusindikwa.

Ongezeko la kazi za kukaa na zisizotumia nguvu.
Tofauti na siku za nyuma, vijana wengi wa sasa hawafanyi shughuli za kutumia nguvu sana. Vijana wengi wanajihusisha na kazi kama ya boda boda , udalali, biashara ndogo ndogo,na kazi za ofisini. Kundi kubwa la vijana wanajihusisha na shuhjuli hizi ni vijana hivyo huwapelekea muda mwingi wasiwe wanatumia nguvu na kuwasababishia wasifanye mazoezi kupitia shughuli zao.

Matumizi ya pombe kali na sigara.
Vijana wengi wanatumia vileo vikali ambavyo hupatikana kwa huuzwa kwa bei ya chini. Pombe hizi zimekuwa zikitumiwa na vijana wa kipato cha chini kwa sababu ya gharama yake kuwa chini . Pia sigara zinatumiwa sana na vijana wengi na pia huwaathiri na watu ambao wanaishi nao. Uvutaji wa sigara unaongeza hatari kupata ugonjwa wa shinikizo la juu la kwa zaidi ya mara kumi.

Madhara ya shinikizo la juu la damu
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu hauna dalili za moja kwa moja hadi madhara yake yanapojitokeza baada ya muda mrefu. Ugonjwa huu usipogundulika mapema na kuanza tiba yake unaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya hata kifo cha ghafla.
Madhara ya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ni kiharusi (stroke),matatizo ya moyo, kupasuka kwa mishipa ya damu kwenye ubongo (cerebrovascular accident), figo kushindwa kufanya kazi (chronic kidney failure), kuharibika kwa mishipa mikubwa ya damu (aortic aneurysm) na mengine mengi.
Baadhi ya mitindo ya maisha ambayo inaweza kuondoa vijana kwenye hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu ni kama ifuatavyo

Kupunguza matumizi ya chumvi
Kwa kuwa chumvi nyingi (hasa chumvi mbichi) ni kisababishi cha ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, tunaweza kupunguza hatari ya ugonjwa huu kwa kuweka sera ya kuhamasisha kitotumia chumvi mbichi. Mfano sio lazima kuongeza chumvi kila ukiangiza supu hotelin au viazi vya kukaanga (chips). Vile vile hakuna ulazima wa kuchovya kwenye chumvi unapokuwa unakula nyama choma au mihogo. Kama vijana wengi wataacha kutumia chumvi mbichi kwa namna hii hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Kupunguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi
Inawezekana kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama soda na vinywaji vingine vya kusindikwa. Ikiundwa sera ya kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi kutapunguza sana hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu. Mfano wizara ya afya inawezekana kuanzisha kampen ya unywaji wa maji badala ya soda na juisi, ulaji wa vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi na ulaji wa matunda halisi badala ya juisi ya matunda hayo itamsaidia sana kupunguza kiwango cha sukari kinacholiwa na watanzania kwa nyakati hizi.

Kudhibiti matumizi ya pombe na sigara
Hatari ya kuathirika na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu inaweza kupungua ikiwa watu watadhibiti matumizi ya pombe na sigara. Tunaweza kudhibiti matumizi haya kiwaelimisha watu kuhusu kiwango cha pombe kinachotakiwa kunywewa kwa siku. Kwa kuwa vijana wengi hasa wa kipato cha chini wanakunywa pombe kienyeji na kali za viwandani, serikali inapaswa kudhibiti uzalishaji wa bidhaa hizo. Pia sigara zisivutwe kiholela kila sehemu bali kuwepo na maeneo maalum ya kuvutia sigara badara ya kuvutia kwenye mikusanyiko kama sokoni na barabarani kiholela ili kuwalinda wasiovuta sigara.

Kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara
Watu ambao hawana muda wa kufanya mazoezi wanaweza kufundishwa kufanya mazoezi kwa kutembea au kuendesha baiskeli wakiwa wanaenda kwenye shughuli zao .Pia kuna mazoezi mepesi ambayo mtu anaweza akafanya mwenyewe akiwa chumbani kwake na watu wanaweza kufanya hivyo baada ya kufundishwa na kuhamasishwa pia.

Kuhamasisha upimaji wa afya mara kwa mara na kuanza matibabu mapema
Vijana wengi hasa wa kiume hawana tabia ya kupima hali zao za afya mara kwa mara katika jamii zetu. Iwapo vijana watakuwa na tabia ya kupima afya zao hasa shinikizo la damu, itawasaidia kujua hali zao na wale watakaogundulika wataanzishiwa matibabu ili kuepusha madhara yake.

Hitimisho
Ili tuweze kuipata Tanzania iliyo imara miaka 25 ijayo na baadae, tunahitaji vijana wenye afya njema sasa ambao watakuwa wazee wenye afya hapo baadae ambao wataendelea kuwa na mchango kwenye jamii na kutengeneza kizazi bora cha miaka mingi ijayo. Ikiwa ugonjwa wa shinikizo la juu la damu utadhibitiwa, magonjwa mengine yasiyokuwa ya kuambukizwa kama kisukari, tezi dume, matatizo ya uzazi na mengineyo yatakuwa yamedhibitiwa pia hivyo tutakuwa na jamii yenye afya bora.
Nzuri Sana hii mkuu
 
Thanks for your education promotion
 
Back
Top Bottom