Wakuu kuna DJ moja alikuwa anaitwa Mangapi, je kuna mtu anataarifa zake? Mara ya mwisho kumtia usono ilikuwa mwanzoni mwa 1990, mtaa wa TOGO, Kinondoni A.
Asante sana mkuu taarifa hizi za kusikitisha. May God rest his soul in Peace kwa mchango wake wa kutoa burudani kwa wakazi wa Dar, haswa mitaa ya Kinondoni.
Afro Afro mama ooh mtoto wa Sagana eh mama, salaamuu zangu nakutumia popote ulipo zipokee,
Nisalimie ndugu na wazazi wako mama popote walipo Afro
Mimi sijambo lakini mawazo tele moyoni nina wasiwasi,
Nikikumbuka tulivyoachana mara ya mwisho uliniahidi Afro
Tungeonana mapema siku zinapita bibie mbona sikuoni mama, afro mama ehee mtoto wa Sagana.
Kaa ukumbukee mama penzi hugeuka, leo kwangu kesho kwako, utanikumbukaa
....