Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Yaani chama chetu cha Mapinduzi CCM sijui kina matatizo gani, hakuna kiongozi anayeweza kusimama akataka jina la Mama akaacha kutaja Madarasa. Hivi kuna kubwa zaidi ya hili? Hakuna mradi wowote alioanzisha Mama umegharimu zaidi ya Trilioni 1.3?
Tunasahau kuwa kuna watu walijenga shule za kata nchi nzima kwa muda mfupi? Mbona hapakuwa na fujo hizi za kusifia mpaka kupitiliza? Kwanini tunasahau kuwa vituo vya afya bado ni tatizo kubwa na maji safi na salama bado tatizo ni kubwa, tumesahau kuwa tatizo la ajira nchini ni kubwa kiasi gani?
Hawa hawa wanaotembea na mabango barabarani wakisifia madarasa, madarasa, ndio hawa hawa awamu iliyopita ilikuwa flyover, flyover, ndege, ndege. Leo hii huwezi kukuta mtu anazungumzia flyover wala ndege, miradi ambayo kimsingi ni mikubwa kuliko haya madarasa.
Mama atiwe moyo kwa mambo mengi anayofanya na siyo kusifia tu kwa jambo moja, tusijisahau shida za watanzania ni nyingi kuliko haya madarasa.