Wimbo wa kilatini ulioimbwa siku ya ibada ya kumuaga Hayati J.K Nyerere pale st. Joseph tarehe 19 October 1999

Wimbo wa kilatini ulioimbwa siku ya ibada ya kumuaga Hayati J.K Nyerere pale st. Joseph tarehe 19 October 1999

Joined
Mar 3, 2022
Posts
27
Reaction score
40
Ilikuwa ni siku ambayo jiji la Dar es salaam liligubikwa na majonzi huku vilio vikitawala katika kila kona yake. Majonzi haya hayakutokana na kumpoteza mwasisi wa nchi hii pekee bali ni hofu ya watu wengi kuhusu mustakabali wa nchi hii bila kuwepo Kwa mzee huyu aliyeonekana kuwa ni kielelezo na ishara ya uzalendo wa nchi hii.

Mengi yalionekana, yakasemwa na kunong’onwa. Ya kweli na yasiyo ya kweli. Ama hakika nilijifunza mengi katika umri wangu mdogo niliokuwa nao.

Siku hii baada ya kufungua kinywa mama aliongozana na mm mpaka kanisa kuu la mtakatifu yosefu posta. Katika ibaada mambo mengi yalikuwa tofauti sana na utaratibu wa ibaada za kikatoli za kuaga marehemu. Kwa kawaida Rangi ya urujuani hutumika Kwa mavazi ya kiongozi wa ibaada na matandiko yote lakini ile siku rangi nyeupe ilitumika. Nyimbo za utukufu na Alleluya haziimbwi lakini siku ile ziliimbwa na pia halleluya kuu ikaibwa.

Kubwa zaidi ni wimbo wa kilatini maalumu ambao uliimbwa wakati mwili wa Hayati Nyerere ukiingizwa kanisani. Wimbo huu nmekuja kuusikia mara ya pili katika ibaada ya mazishi Papa Yohanne Paulo II.

Mwenye kuufahamu wimbo huu aniambie unaitwaje, na unapaswa uimbwe maalumu Kwa ibaada za mazishi ya watu gani na kwanini? Na ikiwezekana uwekwe hapa.
 
Back
Top Bottom