Wimbo wa mwisho wa Franco

Shukrani sana mkuu lucas mobutu.ila huyu mzee wanasemaga alidedi kwa HIV.

Na miaka hiyo wanamuziki wengi sana waliondoka na maradhi hayo,ila tusihukumu!
 
yaal mwaka 73, ndio alikufa bavon Marie cc@masiya
Bavon Marie Marie (Siongo Bavon) alifariki August 5, 1970 akiwa kijana wa miaka 26. Anaetaka kufahamu alikufaje amtafute Mzee Tshimanga Assosa (Papa Tshim) ambaye walikuwa wote siku msiba ulipotokea na alikuwa rafiki yake Bavon wakiwa wote bendi ya Negro Success. Bavon alikuwa mdogo wake Franco na kama kaka yake alikuwa Mpiga solo maarufu DRC akiwa na Mzee Bholen (nae marehemu) ambaye pia alikuwa mpiga solo na kiongozi wa Negro Success.
 
Hapana mkuu wa mwisho ni les rumeurs. Hata ukizisikiliza utagundua kua saut ya Franco kwenye les Rumeurs imeisha.na pia uli achiwa miaka 3 baada ya kifo chake

Kweli kabisa,sauti yake katika huu wimbo dhahiri aliuimba akiwa katika hali dhoofu kiafya (by the way wimbo wenyewe si ndio huu ambao jamaa ameandika mashairi yake hapo juu?)
 
mkuu lucas mobutu huu wimbo unataka kufanana na ule uitwao "makambo ezali minene" una maudhui sawa na huu ninazo tafsiri za nyimbo za Franco nyingi tu sema sijui namna ya Ku attach hapa
cc Masiya
Makambo ezali ya minene au makambo ezali ya Bourreau ni kuhusu matatizo ya mapenzi na les rumeurs ni kuhusu umbea hata kifo walimtangazia hata hajafa.
 
RIP La Okanga La ndju Pene Lwambo Lwanzo Makiadi aka Franco. Miaka nnakua na kupata fahamu hizi nyimbo ndo zilizokuwa zinatamba sana. Tulikuwa na santuri na kanda nyingi tu za Franco. Nyimbo zake ni tamu balaa, halafu kuna watu walipitia pale TP ok Jazz ilikuwa km chuo flani, Lutumba Simaroo Masiya, Youlou Mabyala, Madilu System, Josky Kiambukuta hawa watu walipikika haswa. Sikiliza Freins a Man! Lwambo Noma
 
Safi sana. Kuna jamaa nilikuwa nikisikiliza nyimbo zake, jina nakumbuka alikuwa anaitwa PAPA MIKI. siku hizi nikijaribu hata kwenye internet sioni jina hili, ukiachilia kupata nyimbo zake, kulikoni?
 
Kweli kabisa,sauti yake katika huu wimbo dhahiri aliuimba akiwa katika hali dhoofu kiafya (by the way wimbo wenyewe si ndio huu ambao jamaa ameandika mashairi yake hapo juu?)
Ndio huo nimeandika mashairi ,mkuu
 
Makambo ezali ya minene au makambo ezali ya Bourreau ni kuhusu matatizo ya mapenzi na les rumeurs ni kuhusu umbea hata kifo walimtangazia hata hajafa.
Mkuu umewahi iskia la reponse de mario ? Kali sana
 
Ngoja niutafute
 
Safi sana. Kuna jamaa nilikuwa nikisikiliza nyimbo zake, jina nakumbuka alikuwa anaitwa PAPA MIKI. siku hizi nikijaribu hata kwenye internet sioni jina hili, ukiachilia kupata nyimbo zake, kulikoni?
Huyo sijamsikia
Ila nyimbo nyingi za zamani ukizitaka ingia youtube au lingala instute ndio utazipata na tafsiri zake
Hazipo mitandao mingi sababu wasikilizaji hamna
 
shukrani kwa ufafanuz napenda mno nyimbo za rhumba
 
shukrani kwa ufafanuz napenda mno nyimbo za rhumba
Mkuu umewahi iskia la reponse de mario ? Kali sana
ile si.n remix ya Mario?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…