Wimbo wa 'Ni wajibu Kumshukuru Baba Nyerere' wa Hayati Capt. John Komba, hauchujagi

Wimbo wa 'Ni wajibu Kumshukuru Baba Nyerere' wa Hayati Capt. John Komba, hauchujagi

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Wimbo wa NI WAJIBU KUMShuKURU BABA NYERERE WA HAYATI Capt. JOHN KOMBA, HAUCHUJAGI

Tukielekea katika kuadhimisha kumbukizi ya maisha, kazi na kifo cha hayati Baba wa Taifa Oct 14ijayo,

Hebu pata muda kidogo sikiliza wimbo huu muhimu sana usiochuja, ulio jaa vionjo vyenye hisia kali, tafakari na ujumbe mzito na wa maana sana kwa waTanzania wote, lakini kwa ufupi pia, ukieleza maisha ya Mwl. J.K.Nyerere binafsi na jitihada zake katika kulijenga Taifa huru la Tanzania, na siri ya umoja, amani na utulivu huu wa wananchi na waTanzania kwa ujumla.

Hakika tunao wajibu kama Taifa, wa Kumshukuru Mungu kwa Zawadi ya Maisha ya Uongozi wa J.K.Nyerere, waziri mkuu na raisi wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Asante sana hayati Capt. J. Komba kwa kumbukumbu ya wimbo huu mzuri na wa maana sana kwa vizazi na vizazi kujifunza na kujua mengi zaidi kwa kifupi kuhusu hayati Baba wa Taifa kupitia wimbo huu maalumu..

Mungu Ibariki Tanzania..

R.I.P Capt.John Kombo
R.I.P Baba waTaifa J.K.Nyerere
 

Attachments

Ngoma kali sana hyo
Carasco,
Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika mikutano ya kwanza ilifanyika Mnazi Mmoja leo ni pale mbele ya Chuo Cha Watu Wazima.

Kabla Julius Nyerere hajapanda jukwaani Sheikh Suleiman Takadir alikuwa anatangulia na anasoma dua na watu wote wanaitika.

Kisha atamtambulisha Nyerere.

Baada ya hapo akina mama wakiongozwa na Bibi Titi na Hawa bint Maftah wataimba nyimbo hiyo hapo chini:

"Muheshimiwa nakupenda sana
Wallah sina mwinginewe
In Shaa Allah Mungu yupo
Tanganyika tutajitawala."

Nyerere atapanda jukwaani na kuhutubia wananchi.

Hii nyimbo alikuwa akiimbiwa Nyerere na ndiye mheshimiwa anaetajwa kwenye hiyo nyimbo.

1725306680765.jpeg
1725305339388.jpeg

Hii ndiyo Mnazi Mmoja mkutano wa TANU angalia kushoto utaona sehemu kuwa weusi.
Hayo ni mabaibui wamevaa akina mama na walikuwa na sehemu yao maalum hawachanganyiki na wanaume hapo ndipo zilipokuwa zinatoka nyimbo za lelemama za kumsifia Julius Nyerere na TANU.
(Picha kwa hisani ya watoto wa Mohamed Shebe mpiga picha wa kwanza wa TANU na Nyerere)​
 
Back
Top Bottom