Wanajamvi, nakuja kwenu kutaka msaada kwa wataalamu wa fasihi kuhusu ujumbe uliomo katika wimbo uliotajwa hapo juu. Kiukweli Mrisho Mpoto namkubali sana kwa mashairi yake - tatizo tu sipati ujumbe sababu ya mafumbo yaliomo katika mashairi yake.
Nakuja kuomba yeyote anayeelewa ujumbe uliomo katika wimbo huu anisaidie. Naambatanisha video ya wimbo huo hapa.
Asanteni.