Na huu uliopo sasa baada ya kupata uhuru umetungwa na nani,kuna makala moja niliwahi soma inamaelezo alikuwa Enoch Ngoxhsa aliutunga mwaka 1915 ni raia wa South Africa. Ni kipindi kirefu kwahiyo Sina uhakika. Anae elewa msaada
Mungu ibariki Afrika
Noti za muziki wa nyimbo
Enock Sentonga,mtunzi wa wimbo wa Nkosi Sikeleli Afrika
Mungu Ibariki Afrika ni
wimbo wa taifa wa
Tanzania.
Jina linatokana na
maneno yake ya kwanza.
Asili yake ni
wimbo Nkosi Sikelel' iAfrika wa
Afrika Kusini.
Enoch Sontonga ndiye
mtunzi wake
mwaka 1897.
Sehemu ya wimbo huu inatumika pia katika nyimbo za taifa za
Afrika Kusini na
Zambia. Huko nyuma ulitumiwa kama wimbo wa taifa wa
Zimbabwe.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Afrika Wabariki viongozi wake Hekima, Umoja na Amani Hizi ni ngao zetu Afrika na watu wake
KIITIKIO:
Ibariki Afrika Ibariki Afrika Tubariki watoto wa Afrika Mungu ibariki Tanzania Dumisha Uhuru na Umoja Wake kwa Waume na Watoto Mungu ibariki Tanzania na watu wake
KIITIKIO:
Ibariki Tanzania Ibariki Tanzania Tubariki watoto wa Tanzania
Historia yake kwa urefu
Wimbo "Nkosi Sikelel' iAfrika", yaani "God Bless Africa", ulitungwa na Enoch Sontonga,
Mxhosa,
raia wa Afrika Kusini, na baadaye kutafsiriwa na
kanali Moses Nnauye kwenda
Kiswahili kuwa "Mungu ibariki Afrika".
Ulikuwa wimbo wa
African National Congress (ANC) walipokuwa wanapambana na
ukandamizaji wa
Makaburu.
Pamoja na kutumika katika Afrika Kusini, umeimbwa pia katika nchi nyingine, kwa mfano
Zimbabwe na
Namibia, na labda hata
Botswana,
Lesotho,
Swaziland, na
Malawi kwa miaka mingi.
Hata kabla ya
TANU (Tanganyika African National Union) kuanzishwa mwaka wa
1954, wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulikuwa unaimbwa Afrika Kusini, kama vile chama cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilivyoanzishwa miaka mingi kabla ya chama cha TANU.
Kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika
Bloemfontein ili kuanzisha chama hicho mwaka wa
1912, waliimba Nkosi Sikelel' iAfrika.
Julius Nyerere alikuwa bado hajazaliwa. Chama kilichoanzishwa kiliitwa South African Native Congress chini ya uongozi wa
John Dube, Mzulu, na Pixley ka I. Seme pia kutoka
Natal kama Dube. Kikabadilishwa jina baadaye na kuitwa African National Congress (ANC).
Kuanzia mwaka wa 1925, wana ANC waliuchagua wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, kama wimbo wao wa taifa na bado unaimbwa leo.
Katika nyimbo za mataifa yetu ya Kiafrika, hakuna wimbo mwingine unaojulikana kama wimbo huo. Hata katika nchi za
Afrika Magharibi, watu wengi wanajua Nkosi Sikelel' iAfrika ni wimbo gani na unamaanisha nini. Hata
Kenya wanaimba wimbo huo. Unaimbwa na unafahamika katika nchi nyingi hata kaskazini mwa bara hili. Ukienda
Misri,
Algeria na nchi nyingine huko, utawakuta watu wengi wanaojua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika.
Enoch Sontonga alitoka Eastern Cape Province, jimbo la Waxhosa, ambako pia ni nyumbani kwa
Nelson Mandela. Alitunga wimbo huo kama wimbo wa
Kanisa katika lugha yake ya Kixhosa kama wimbo wa bara lote. Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel' iAfrika, God Bless Africa, si God Bless South Africa.
Alipotunga wimbo huo mwaka wa 1897, haukuimbwa hadharani mpaka mwaka wa
1899. Uliimbwa kanisani kwa mara ya kwanza mwaka huo. Halafu, baada ya miaka
kumi na tatu, uliimbwa kwenye mkutano wa kwanza wa South African Native Congress mwaka wa 1912 uliofanyika Bloemfontein kuanzisha chama hicho kugombea haki za Wafrika.
Hata Watanganyika wengi waliokwenda kufanya kazi
migodini Afrika Kusini
miaka ya 1940 na
1950 waliujua wimbo huo. Walikuwa wanaimba Nkosi Sikelel' iAfrika pamoja na watu wa Afrika Kusini walipokuwa huko na waliporudi
Tanganyika.
Watanganyika wengi, mara baada ya kupata
uhuru, walikuwa au waliona music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika ikiwa na jina la Enoch Sontonga kama ndiye mtunzi wa wimbo huo. Ilikuwa katika lugha mbili, Kiswahili na
Kiingereza, na
kichwa chake kilikuwa Mungu Ibariki Afrika, God Bless Africa, yaani Nkosi Sikelel' iAfrika.
Sikiliza wimbo huo katika
Youtube ambao mmoja wa
waimbaji wake katika
video ni
Miriam Makeba. Ukiusikiliza
muziki wake, hauna tofauti hata kidogo na ule wa wimbo wa taifa, Mungi Ibariki Afrika, au wa wimbo wa taifa wa Zambia.
Nyimbo nyingi za Enoch Sontonga zilikuwa nyimbo za
huzuni kuhusu
maisha magumu ya Wafrika chini ya utawala wa
Wazungu waliokuwa wanawakandamiza Wafrika katika bara lote. Wimbo wake, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulitokana na
maumivu hayo ya Wafrika ingawa pia ulikuwa wimbo wa kuwapa
tumaini kwamba hawako peke yao.
Mungu yuko nao, au yuko nasi, ingawa tunaumia na tunateswa na wanaotutawala kwa mabavu.
Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, uliwekwa kwenye sahani ya
santuri kwa mara ya kwanza huko
London, mwaka wa
1923. Uliimbwa na Solomon Plaatje,
mwimbaji maarufu wa Afrika Kusini ambaye pia alikuwa mmoja wa Wafrika walioanzisha chama cha South African Native Congress, Bloemfontein, mwaka wa 1912.
Ni wimbo wa Watanzania pia kwa sababu Afrika ni moja. Kwa hiyo hawakuiba wala kuazima wimbo huo kwa kuufanya wimbo wa taifa. Ni wa watu wa Afrika Kusini na wa nchi nyingine zote za Afrika vilevile.
Utumizi wa wimbo huo unaonyesha
umoja na
undugu wa Waafrika. Ndiyo maana kulikuwa hata vyama vilivyopigania uhuru ambavyo majina yao yalifanana au yalikuwa karibu sana. Kwa mfano, African National Congress (ANC) iliyoundwa Tanganyika na kuongozwa na
Zuberi Mtemvu na
katibu wake mkuu
John Chipaka ilikuwa na jina sawa na la chama cha Afrika Kusini cha akina Mandela.
Pia chama cha kwanza kupigania uhuru Northern Rhodesia kilichoongozwa na
Harry Nkumbula kilikuwa kinaitwa African National Congress, na kiliendelea kuitwa hivyo hata baada ya wanachama wengine kuondoka na kuunda chama kingine, United National Independence Party (UNIP), chini ya uongozi wa
Kenneth Kaunda.
Kenya kulikuwa na
Kenya African Union (KAU) kabla ya Tanganyika African National Union. Baadaye KAU ikabadili jina kidogo na kuitwa
KANU. Na ndugu zetu Zimbabwe waliunda chama kinachoitwa
ZANU baada ya baadhi yao, pamoja na
Robert Mugabe, kuondoka na kuachana na
ZAPU.
Majina hayo, katika nchi mbalimbali, yanafanana kwa sababu Waafrika wanajiona na kweli ni ndugu, bila kujali
kabila,
rangi,
dini, au
asili. Pia inaonyesha
ushirikiano wao. Hata
Uganda,
jeshi lao ni Uganda People's Defence Forces (UPDF), jina linalotokana na jina la Tanzania People's Defence Forces (TPDF).