Wimbo wa Tazama Ramani

Wimbo wa Tazama Ramani

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
1. Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2.

2. Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2

3. Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha X2
 
Mnaaharibu wimbo

Nafaka - faa

Hapa ni

Kila Mara kwako niwe nikiburudika.

Hebu jaribu tune uone km utaweza kuimba km ulivoandika na wew.
Nilikuwa sijui mkuu shukrani mpendwa me kila siku najua Ni mabonde ya nafaka yaani means ardhi inayofaa kwa kilimo
 
Huu wimbo siku hizi umebadilika?
Nakumbuka kiitikio cha verse ya pili ni " majira yetu haya yangekuwaje sasa utumwa wa nchi TANU imeukomesha" na verse ya mwisho ni " ... utumwa wa nchi Karume ameukomesha"
 
Daah huu wimbo umeniokoa sana
Nikikuwa mahali nikaambiwa niimbe nimeugoogle chap
 
Back
Top Bottom