March 7 mwaka 1985 baadhi ya wasanii waliounda kundi la “USA for Africa” walitoa kibao cha We are the World.
Lengo kuu la wimbo "We Are the World" lilikuwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia waathirika wa njaa na umaskini uliokuwa ukiathiri sana nchi za Afrika, hasa Ethiopia, katika miaka ya 1980.
Inasadikika watu takribani Milioni 1 walipoteza maisha kwa baa la njaa la mwaka 1984 na 1985 huko Ethiopia.
Wimbo huu uliandikwa na Michael Jackson na Lionel Richie, na ulirekodiwa mwaka 1985 na kundi la wasanii mashuhuri wa Marekani waliounda kikundi kilichoitwa USA for Africa (United Support of Artists for Africa).
Malengo Mahususi ya wimbo huu yalikuwa:
Kuelimisha dunia kuhusu janga la njaa Afrika, hasa Ethiopia, ambako maelfu ya watu walikuwa wakikumbwa na baa la njaa.
Kuhamasisha mshikamano na utu wa kibinadamu, kwa kuonesha kuwa watu kutoka mataifa mbalimbali wanaweza kushirikiana kwa ajili ya kusaidia wenzao walioko katika hali ngumu.
Kukusanya fedha za misaada ya chakula, dawa, na mahitaji mengine muhimu — mapato kutoka mauzo ya wimbo huu yalipelekwa moja kwa moja kusaidia Afrika.
Kwa ujumla, wimbo huu ulikuwa ni mfano wa jinsi sanaa na muziki vinaweza kutumika kama chombo cha kubadilisha jamii na kusaidia watu walioko katika matatizo makubwa.
Wasanii waliohusika ndani ya wimbo huu ni;
Lionel Richie
Stevie Wonder
Paul Simon
Kenny Rogers
James Ingram
Tina Turner
Billy Joel
Michael Jackson
Diana Ross
Dionne Warwick
Willie Nelson
Al Jarreau
Bruce Springsteen
Kenny Loggins
Steve Perry
Daryl Hall
Huey Lewis
Cyndi Lauper
Kim Carnes
Bob Dylan
Ray Charles
Tuambie kwa mara ya kwanza wimbo huu uliusikia mwaka gani?
Hehe! kawimbo tu kamenichapa miaka kibao kinyama!, halafu nikiambiwa bado nanuka maziwa ati nakaza fuvu!..
Najikuta mimi ndio mimi mla mishangazi badala nitulize kizazi mimi ndo kwanza nakichakaza!, kwa hili wacha nijitafakari aisee..🤣