Winfrida Hubert Gerald(16)🇹🇿 One of the Best Talent

Winfrida Hubert Gerald(16)🇹🇿 One of the Best Talent

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
WINFRIDA HUBERT GERALD(16)🇹🇿 One of the Best Talent 🧠! Kuanzia ndani ya klabu yake ya JKT Queens hadi National Team za Wanawake amekuwa na kiwango bora sana uwanjani pale anapopata muda wa kucheza, yupo kwenye umri sahihi kabisa wa kucheza soka la ushindani hasa ukitazama daraja la Ligi Kuu anayocheza na muendelezo wake

Michuano hii ya U17 GIRLS INTEGRATED FOOTBALL TOURNAMENT 2025 ambayo inaendelea pale Dar Es Salaam binti yupo kwenye kiwango cha juu sana! Kuanzia mechi ya kwanza hadi ya tatu leo JKT Queens wameshinda mechi zote, wamefunga jumla ya magoli 15 na kufungwa moja pekee huku Winfrida Gerald akifunga magoli sita kati ya hayo

Tazama akicheza kama kiungo mshambuliaji atakupa uwiano mzuri ndani ya uwanja kama ambavyo atacheza akiwa mshambuliaji wa mwisho, uwezo wake wa kukimbia na mpira eneo kubwa la uwanja upo juu hapo hujasema kuhusu nguvu kisha kasi na ufanisi wake mbele ya 18! One of the Best, Winfrida Hubert Gerald 👑💪

Let's Goo!!.
 
Bora umemuona huyo Binti ni hatari sana tangu akiwa fountain gate girls
Naamini atavuka walipofika kina Aisha na Opah
 
Back
Top Bottom