Winston Churchill Waziri Mkuu wa Uingereza aliyekubalika na watu wengi

Winston Churchill Waziri Mkuu wa Uingereza aliyekubalika na watu wengi

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari!

Mr Wiston Churchill ni moja ya muingereza maarufu kipindi cha karne ya ishirini na aliingoza uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia.

Wiston Churchill alizaliwa mnamo 1874 na kupata nafasi bungeni mwaka 1900. Alikuja kuwa waziri mkuu ‘British Prime Minister’ kuanzia mwaka 1940 – 1945 na kwa mara nyingine tena mwaka 1951 – 1955.

Churchill anakumbukwa sana kwa kufanikiwa kuliongoza taifa la Britain vyema wakati wa vita vya pili vya dunia. ‘World War Two’. Sambamba na umaarufu wa kuwa na hotuba bora za kuhamasisha kutokata tamaa japo odds hakikuwa upande wake nikiwa na maana ya mambo kwenda ovyo.

Alitambulika kama shujaa wa muda wote kwa taifa la uingereza pia alikuwa na hotuba zilikuwa zimebeba masirahi ya taifa hilo ambazo zimekuwa historia na zitadumu kwa kipindi kirefu, japo kuna maamuzi mengine aliwahi kufanya yaliacha mshangao hadi sasa kwa watu. Kadharika Sanamu nyingi za Mr Wiston Churchill zilimejengwa sehemu tofauti tofauti mijini huko ikiwemo nje ya bunge la Uingereza.

Alijipatia heshima hadi leo, wanaendelea kumuenzi na kumkumbuka kwa maamuzi yake ya kutokata tamaa kipindi cha vita ya pili ya dunia dhidi ya jeshi la kijerumani (Nazi)

Pamoja na yote hayo Mr Wiston Churchill alisumbuliwa na matatizo ya kiafya ya akili tuweza sema ‘Mental Health Problems’ yaliyosababisha kufanya baadhi ya mambo ya ajabu ajabu sana kwenye maamuzi yake ambayo hadi sasa hakuna mtu ambaye angeyapenda kufanya au kufanyiwa.

Watu wengi wanaamini ndiye muingereza jasiri wa muda wote wa uingereza na ndiye waziri mkuu aliyejichukulia umaarufu hadi sasa toka waziri wakuu wengine kupita.

Kabla ya vita vya pili vya dunia mnamo 1939, Mr Wiston Churchill aliwahi kuzungumza juu ya kuibuka kwa Hitler na Nazis huko Germany na kuonya kuwa ni tishio kwa mataifa mengine ikiwemo Uingereza.

Kipindi anakuwa waziri mkuu wa uingereza mnamo 1940 ni baada ya waziri mkuu aliyepita Neville Chamberlain kujiudhuru.

Churchill alikataa kata kata ku-surrender kwa majeshi ya ujerumani (Nazi) na hicho ndicho kilichowavutia wengi kwenye taifa la uingereza.

Churchill alikuja kupoteza madaraka yake ya uwaziri mkuu baada tu ya vita vya pili kukoma mnamo mwaka 1945 japo alikuja kupata madaraka tena ya uwaziri mkuu wa uingereza 1951 na baada ya miaka mnne mbele alijiudhuru.

Matatizo ‘Mental Health Problems’ aliyokuwa nayo Churchill kwa kipindi kirefu japo alikuwa ni waziri mkuu bora wa muda wote kwa watu wengi ila alikuwa na mambo yake yaliyokera wengi. Mental disorder kuwa mtu mwenye depression ambacho Mr Churchill mwenyewe aliupa jina kama ‘the black dog’. Rafiki wa Churchill aliwahi kueleza kuna kipindi Mr Churchill anaweza kuwa mwenye kujiamini sana wakati wa kufanya maamuzi ila kuna wakati anaweza kuwa mtu ambaye anabadirika badirika asiyeeleka kwenye kufanya maamuzi yake mwenye na asijue nini cha kufanya kabisa na hapo alikuwa na tabia ya kufanya vitu visivyoleta mantiki yeyote.

Kuna mijadara mingi ambayo hadi sasa imeendelea kutoka na maamuzi pamoja na mambo alikuwa anayaamini kwa ujumla na hotuba zake zimeleta mijadara kadha wa kadha.




Itaendelea……

Nawasilisha Mzee Mkoloni

Cc: Kichwa Kichafu
Mr%20Churchill.jpg


Mr%20Churchill.jpg
 
Back
Top Bottom