Radium
JF-Expert Member
- Aug 5, 2022
- 489
- 869
Kweli sio jambo zuri kuuchukia muonekano wako. Mtu mzima na heshima zake, hapaswi kutembea huku akijishtukia kuhusu umbo la pua yake ya kwamba watu watalitambua na kulizingatia. Au mdada mzuri kabisa awe anatembea mtaani huku akisikitishwa na jinsi nywele zake zinavyoshuka au jinsi alivyo na vinyweleo chini ya pua.
Lakini, lazima itokee. Unashika kioo au hata kama hutaki basi kwenye madirisha ya majengo unapata kuona kile kinachoakisiwa kuwa ndio wewe, kisha unajiuliza, "KWANINI KATIKA UWEPO WANGU WA MUDA MFUPI KABISA KWENYE DUNIA HII, IMEBIDI ETI HIKI NDIO KIWE MIMI?"
Pua mbaaya, nywele haziridhishi...tone ya ngozi ni mbaaya na kikubwa kabisa, kitu tunachokijua kuliko vyote USO WA KINYONGE ULIOSHUKA NA KUUMBIKA KWA JINSI PEKEE AMBAYO HATUKUITAKA.
Kwa wale wanaojichukia kila picha ni maumivu, kila tunayopiga inaleta taarifa mpya mbaya.
Lakini huu sio ukichaa, tunajali kuhusu muonekano wetu kwa sababu ya muhimu. Kwa sababu kila mtu anatujudge kwa kuutumia huu muonekano.NDICHO kitu cha kwanza kukitambua kutoka kwetu.
Kuweza kudeal na muonekano wetu tunahitaji kujifunza njia ngumu na ya tofauti. Na huu ni muongozo wa kujifunza kucope na muonekano wako.
#1- Sio binafsi.
Katika mamia ya vitu ninavyotumia kukujudge ni kumi rafiki yangu atavitumia kwako huku akiongeza vyake nisivyotumia. Muonekano kwa jamii ya sasa ni kigezo kidogo mno katika demokrasia ya maisha.
NI KAMARI NA HAUJASHINDA.
Huna cha kufanya na mimi sina cha kufanya juu ya muonekano wako. Ni hivyo imeshakuwa.
#2- Makasiriko yako ndiyo chachu ya upendo.
Ni mwanaume mwenye kipara(walaza) atakayezipenda na kuzitukuza nywele zako kuliko mwanadamu yeyote yule.
Ni watu wabaya pekee walio katika nafasi ya kuona uzuri na kufurahisha macho yao.
"Jambo ambalo, hao wazuri waliweke akilini mwao kila wanapofikiria kuhusu aliyewapa hiyo favor"
#3- Tegemea wazazi wako WABAYA.
Mfumo wetu wa kupenda huwa mara nyingi tunajifunza kutoka kwa wazazi wetu tukiwa watoto.
Na tukikua huwa tunatafuta mwenza ambaye anatukumbusha walau kidogo kuhusu wazazi wetu, na ukweli mbaya ni kuwa wengu tuna wazazi wenye muonekano Mbaya ni basi tu tunawapenda na hatushughuliki na mionekano yao.
Utasikia wanaume wakisema wanataka mke wa kawaida kwa sababu ni mvumilivu na rahisi kuishi naye lakini ni reflection za wazazi. Afadhali ya hao kwa sababu wanaooa wake wazuri bado hawajawakimbia wazazi wao completely. Wamefanya hivyo katik physical appearances ila wanaangukia wenza wanaowakumbusha EMOTIONAL TORTURE, DISTANCE AND NEGLECT.
Unfortunately haya machaguo yanafanywa na unconscious mind so utajikuta tu umeangukia pua.
"Thank GOD for UGLY parents"
#4-Staajabu mashujaa wabaya.
Dunia inaongozwa na imetawaliwa na mfumo wa matabaka ya kifedha yasiyo ya haki(Money hierarchy)
Lakini cha kufurahisha ni kuwa kuna Looks hierarchy na katika hii mashujaa wote wa kihistoria wanaangukia pua.
#5- Vumilia bado kidogo.
Bila kujali ni kwa kiasi gani mgawanyo wa mionekano hauko sawa (fair) wakati huu, muda utaleta usawa.
Hakuna anayeishia kuwa na furaha na muonekano wake ni jambo la kusubiri tu.
Kwa wengine jimuonekano baya huanza wakiwa na miaka 10, wengina huo muonekano mbaya husubiri kwa miaka mingine 40. Lakini jambo moja ni uhakika, lazima waishie kuwa wbaya tu.
#6- Tafuta uzuri kwenye sehemu zingine.
Badala ya kusema muonekano haujalishi, anza kuutambua uzuri kwenye part zisizo common.
Tatizo la tamaduni yetu, sio kwamba tunajali sana kuhusu muonekano ila ni kwamba tunafocus katika wigo mdogo sana wa vitu vya kuangalia huku tukipuuza vingine ambavyo pia hubeba urembo maridadi.
Kwahiyo badala ya kuishia kutambua kuwa ana komwe tambua pia kuwa ana macho mazuri yasiyo na mfano, uso wenye uamninifu na ngozi yenye afya.
Kuna mengi mazuri ya kuona katika nyuso za wanadamu wenzetu kama hatutajudge vitu vichache kama tulivyozoea. Huenda siku moja sehemu fulani, mtu mwingine atafanya hivyo na kwetu pia.
## Kabla ya kupinga nisisitize kuwa mengi huwa tunayahisi unconsciously (bila kujua) na sio kila mtu anachukia muonekano wake.
*Wewe unachukia nini kuhusu muonekano wako?
*Ni njia gani unatumia ili ujikubali kuwa ndio uko hivyo?