Wiston Mogha
Senior Member
- Feb 13, 2014
- 168
- 141
WISTON MOGHA AJITOSA KWENYE UBUNGE KIGOMA MJINI (Kigoma Tuitakayo)
Na Mwandishi wetu
Ally Mahmoud
Wiston Mogha amesema ameamua kugombea nafasi hiyo ya Ubunge baada ya kugundua kero nyingi katika Jimbo hilo zimeshindwa kutatuliwa. Alisema ameamua kugombea Ubunge kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Wananchi ikizingatiwa kwamba ipo ndoto ya kufikia malengo ya Kigoma tuitakayo ambayo bado Wawakilishi waliopo sasa wameshindwa kuifikia, lakini anaamini yeye (Mogha) ataweza kufanya haya yaliyowashinda wengi.
Amedai kuwa Mbunge wa sasa (Zitto Kabwe) ameshindwa kuleta mabadiliko ya Mji wa Kigoma Ujiji na matokeo yake hali ya kiuchumi kwa Watu inazidi kuwa ngumu licha ya kuzungukwa na fursa za kila aina kama vile Ziwa Tanganyika, ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo na Changamoto za wafanyabiashara huku jimbo letu likiwa ni sehemu ya eneo la kimkakati kati ya Nchi ya Congo na Burundi.
Anasema akifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini atahakikisha anaibana Serikali kutangaza vivutio vya Ziwa Tanganyika ikiwa ni pamoja na kutafuta Wawekezaji katika sekta ya uvuvi ili walete Meli za kuvulia Samaki, hivyo kufikia malengo ya kujenga kiwanda cha kusindika Samaki Mjini Kigoma. Kujengwa kwa Kiwanda cha kusindika Samaki kutaongeza fursa ya ajira kwa Wananchi kiasi kwamba itasaidia kupunguza wimbi la Vijana kukimbilia katika Mikoa mingine kutafuta ajira.
Hata hivyo amesema Mbunge wa sasa hakuwa na mahusiano mazuri na Madiwani wengi ambao ndio walikuwa wanaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mpaka kuamua kumkimbia, pia hajui shida za Wananchi kwa kuwa ameshindwa kufanya mikutano ya hadhara na badala yake amekuwa akivizia ziara za Viongozi wa Kitaifa kuongea na Wananchi.
Mogha ameomba ridhaa ya kugombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi. Wakati Mogha akieleza nia yake aliyodai haikutokana na kuombwa au kushurutishwa na yeyote, amesema amejipanga vizuri kukabiliana na Mtu au Watu watakaojitokeza kuanzia kura za maoni ndani ya Chama chake na hata Uchaguzi mkuu wenyewe kwa kukabiliana na Wagombea wa Vyama vingine vya siasa.
Wiston Mogha akiwa anaongea na mwandishi wetu amesema kwanza anaomba Uzima wa afya na pia anawashukuru sana vijana wenzake kumuonyesha anaweza kugombea 2020 Katika jimbo hilo na demokrasia ni Kushindana na si kushindana tu bali ni kuleta Maendeleo kwa Wananchi.
2020 ni zamu ya kizazi kipya (TeamKeshoNyingi)....alimalizia kwa hilo.