Mwita Waitara ni mwanasiasa kutokea nchini Tanzania. Kwa sasa Waitara ni mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini anayemaliza muda wake kwa tiketi ya CCM, awali amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ukonga mwaka 2015 kupitia tiketi ya CHADEMA.
Madai
Julai 12, 2025 kumeibuka kipande cha video kikimuonesha mbunge wa Tarime vijijini anayemaliza muda wake, Mwita Waitara aikimwaga machozi mbele ya waandishi wa habari na kuelezwa kuwa tukio hilo linakuja mara baada ya yeye kukatwa jina na wajumbe.
Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu mchakato wa kutafuta wagombea wa ubunge, udiwani na baraza la wawakilishi kwa chama cha mapinduzi kuzinduliwa rasmi.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa kipande hicho si cha hivi karibuni.
Kipande cha video kinachomuonesha Mwita Waitara mbunge wa Tarime Vijijini akilia si ya mwaka 2025 na haihusiani na mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2025.
Kipande hicho cha video ni kutoka katika sehemu ya hotuba aliyoitoa WaitaraMachi 28, 2023 alipokuwa akizungumzia adha ya migogoro ya mipaka Jimboni mwake.
Mkuu, sasa unaweza kurudi kuniita tena chawa niliepofushwa. Tuliwaelezeni kuwa wajumbe wa Halmashauri za wilaya na mikoa hawana mamlaka ya kukata mtu, bali wanatoa maoni na mapendekezo yao.
Sasa uliesema kakatwa jina limerudi, jifunze kusikiliza na kuheshimu mawazo mbadala hata kama hayaendani na unachoamini.
Mkuu, sasa unaweza kurudi kuniita tena chawa niliepofushwa. Tuliwaelezeni kuwa wajumbe wa Halmashauri za wilaya na mikoa hawana mamlaka ya kukata mtu, bali wanatoa maoni na mapendekezo yao.
Sasa uliesema kakatwa jina limerudi, jifunze kusikiliza na kuheshimu mawazo mbadala hata kama hayaendani na unachoamini.
Kwanini, Mabadiliko ya Katiba ya CCM hayakuhusisha mamlaka ya Kamati ya maadili na urejeshaji wa wagombea.
Kama taarifa zangu zipo sahihi, kifungu kilichobadilishwa ni kimoja tu katika ibara ya 105 ibara ndogo ya 7 (f), kilichotaka majina yarudishwe matatu tu, nacho kimeomgezewa neno "isipokua pale kamati kuu ya Halmashauri kuu taifa itakapoamua vinginevyo"
Maana yake ni kwamba, Halmashauri kuu imepewa mamlaka ya kurudisha zaidi ya idadi iliyoainishwa katika katiba.
Hata bila mabadiliko kulikua na uwezekano wa jina lake kurudi kama Halmashauri kuu ingeona linafaa kuwepo kati ya majina matatu ya awali, kwasababu wao ndio kikao cha mwisho chenye maamuzi.