Witchcraft diaries

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Tumejulishwa rasmi kuhusu maboresho mengine ya Jamiiforums ndani ya siku 45 zijazo... Ni taarifa rasmi toka kwa Mkuu Melo mwenyewe.... Maboresho hayo yanatokana na maoni ya wadau nje ya forum.. Na pengine ndani ya forum pia.,...

Katika maboresho hayo nasi wa mada zetu hizi za kiroho na za mambo ya giza tutakuja kivingine... Tutakuwa na simulizi za kweli zilizotokea lakini ambazo hazina ithibati za kisayansi, ama zimeacha Maswali mengi kuliko majibu
Simimulizi zitahusu nyanja zifuatazo
.Harakati katika kutafuta maisha
. Kusaka UTAJIRI
. Mahusiano na mapenzi
. Makazi na nyumba za kupanga
. Biashara
. Urafiki na Uswahiba nknk
. Harakati za migodini
. Harakati za baharini
. Kazi za usiku
. Changamoto za mochwari
. Uwindaji nknk
Kila mwenye simulizi ya kweli atakaribishwa

Kama uongozi wa Jamiiforums utaridhia basi kutakiwa na hiyo subforum ya witchcraft diaries
 
Namba 3 hapo ndo naisiburi.
Wanaume nyie ni pasua kichwa sana.
 
We ni mtu muhimu sana jamii forum,sidhani kama unalitambua hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…