MAKANJAMNA
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,138
- 1,514
Nchi yetu inaelekea kuzuri sana.
kutokana na wimbi kubwa la ukosefu wa ajira, vijana na hata wazee wameamua kujiingiza katika shughuli za ujasiriamali. Hili ni jambo zuri kwa kuwa, sasa waTanzania wanaanza kuona faida za kutumia rasilimali zao.
ndani ya miaka kumi, kwa hii kasi tunayoenda nayo, tutakuwa mbali sana, kwa kuwa uchumi wa nchi hukuzwa na wananchi wenyewe na wala sio wawekezaji kutoka nje, kama baadhi ya viongozi wetu wnavyoamini.
wajasiriamali wadogo ni ngazi nzuri sana kuziba pengo kubwa la ukosefu wa ajira. wakisaidiwa na biashara zao kufanikiwa basi ni uhakika kuwa wataweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika pato la nchi.
Wajasiriamali wadogo na wale wanaoanza wanakumbwa na matatizo mengi, likiwemo UKOSEFU WA TAARIFA.
tunajua kuwa taarifa kuhusu soko la bidhaa au huduma yako ni jambo la muhimu sana ili uweze kufanya maamuzi sahihi ya nini cha kuzalisha na kwa kiasi gani. Vivo hivyo, taarifa kuhusu masoko ni muhimu sana katika kupanga bei.
je taarifa hizo zinapatikanaje?? Mojawapo ya njia ya kupata hizo taarifa ni kupitia utafiti wa masoko 'marketing research'
huu ni wito wangu kwa vijana waliomaliza elimu ya vyuo vikuu ambao wanaujuzi katika masuala ya biashara hasa masoko, kuanzisha kampuni ndogo ambayo itatoa huduma hii kwa wajasiriamali wadogo (na wanaoanza) ambao hawawezi kugharamia huduma hii katika kampuni kubwa.
naamini kama 'young junior professionals' katika masoko, hasa wale waliotoka vyuoni karibuni wakiamua kuanzisha kampuni hii hawatakosa wateja kwa kuwa watu wengi sana wanahitaji taarifa na ushauri kuhusu bidhaa wanazozitengeneza.
kuanzishwa kwa kampuni hii kuzingatie bei itakayotozwa kwa wajasiriamali wadogo, kwa kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho katika kupata ushauri na taarifa za kitaalamu ni bei itozwayo na makampuni makubwa.
shime, vijana wa 'marketing' fanyieni kazi wazo hili.