Wito, Kuna Mashindano ya Kombe la diwani huku Tegeta kwa ndevu mshindi anaondoka na bajaji mpya, Tunawaalika Simba sc waandike barua mwisho tar 1

Sidhani kama ni Kashfa Kwa nchi kama unavyosema. Ila haiwezekani Chama cha soka kikaanzisha mashindano mwishoni mwa kalenda ya mwaka ya Soka halafu Wenye busara wakakaa kimya. Muungano unajulikana ni 26 April na maadhimisho ya miaka 60 yalijulikana kitambo, iweje mashindano yaanzishwe ghafla kàma tumbo la kuhara?
 
Nyie mbona kama mmevurugwa.....hahaha tupe barua tuje tushiriki...
 
Mangungu na try again wapewe 5 Tena kwa maana wamevunja rekodi ya mafanikio kwa kubeba kikombe Cha muungano na milioni 50 juu!
Iyo itaongezeka kwenye mafanikio ya klabu ya msimu mzima baada ya wasap channel kuongoza kwenye mafanikio ayo! Milioni 50 wataweza kushusha vyuma vya maana kwenye usajili wa wachezaji ikiwemo kuwaongezea mikataba kina jobe na fred timu iwe tishio!
Mangungu na try again Amna baya pigeni kazi na mjumuike na wenzenu kupokea kikombe icho kikubwa kabisa kitapowasili pale bandarini kikitokea Zanzibar!
 
Msimu huu kulikuwa na matumaini makubwa kuwa mojawapo au timu zote mbili za TZ kufika mbali katika mashindano ya CAF. Nadhani sababu kuu ya ratiba kutopangwa mapema ni ratiba ya CAF. Nia ya kuyarudisha mashindano ya Muungano ilishawahi kutangazwa miezi mingi iliyopita kwa hiyo chini kwa chini naamini mazungumzo na maandalizi yalikuwa yanafanyika.

Kama Simba+/Yanga ingevuka hadi hatua ya nusu fainali kwenye CAFCL ina maana mashindano haya ya Muungano yangegongana na mechi za nusu fainali CAF.

Labda useme baada ya hizi timu kutolewa tu ratiba ingetangazwa ila hapo bado tunaongelea kama wiki 3 tu zimepita kwa hiyo tunarudi pale pale tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…