Serengeti Highway ijengwe, na ukweli ni kwamba tunapoteza muda kusemasema maneno badala ya kupeleka magreda huko! Hakuna mahali popote dunuiani ambapo watu waliona umuhimu wa kiuchumi katika kufanya jambo wakaacha mradi huo eti kulinda nyumbu na mamba. Ukisikilza sana maneno ya watu ipo siku utakuwa hufanyi kitu. Reli na/ama barabara kuunganisha Arusha na Mara ni mpango mzuri kiuchumi. Peleka magreda huko leo. Maneno maneno maneno mpaka lini?
Hivi watanzania tutajifunza lini kuwa maneno maneno yana ukomo wake wa tija? Kwenye soka--maneno maneno maneno nothing doing in the field; haya: Economics--maneno maneno maneno inflation inahit 20%.
Eti Kenya is the strongest economy in East Africa! Kisa? they are taking action wakati sisi , ambao in reality ndio tunatakiwa kuwa strongest economy kwa sababu ya endowments, tunaendelea na maneno maneno maneno. Damn it! Peleka magreda Serengeti leo!
Kuna ndugu anajiita Inzi anasema tutaathiri eti tolerance level ya wanyama--kwa hivyo panaweza kuja hatari ya wanyama kutoweka. Wanyama wenye akili wata-adapt, wajinga watatoweka kama dinasour, ndege dodo na wengine. Sisi wenyewe ni wanyama, na ndo tupo katika process ya ku-adapt hivyo. Jenga serengeti tupunguze dhiki kwa watu wa mikoa ya ziwa na kutunisha mapato ya taifa letu kwa ujumla tubaki hai!
Ndugu Inzi (inzi?) hili jina litakuwa si la kweli tu. Anyway, Sijui una habari kuwa Kenya kuna mbuga ya Wanyama inaitwa Tsavo, na kwamba kuna barabara ya lami na reli vinakatiza mbuga ile? Unadhani kwanini Wakenya hawajang'oa ile reli na kubomoa ile barabara vitokavyo Mombasa kwenda Kisumu kama kweli wanajali sana kuhusu hizo tolerance level za wanyama?
Of course lengo la kuunga mkono ujenzi wa barabara za Serengeti si kwa ajili ya kuwakomoa wakenya au kulipa kisasi eti mbona wao wamejenga kupitia Tsavo. Sababu kubwa ni kwamba Tanzania ina maslahi makubwa ya kiuchumi katika hiyo njia ya Serengeti. Basi. Tha't it.
Mkuu hapo sio kweli. Kama ungejua madhara wanayopata wanyama wa Mikumi kutokana na uwepo wa hiyo barabara,husingeandika hayo juu. Wanyama wengi wanakufa sana kutokana na uwepo wa barabara hiyo na kutokana na raia kutozingatia sheria na alama za kwenye kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi.
Kwenye suala la wanyama kuzoea au kuadapt mazingira fulani,ni kweli. Ila kumbuka wao pia wana tolerance limit ambayo ikipitwa ndiyo mambo ya extinction au kuwekwa katika Species Red List ya IUCN. Kumbuka wanyama wengi duniani wametoweka baada ya tolerance limits zao kupitwa kwa kiasi kikubwa. Mfano maarufu ni Dinosaurs.
Hapa simaanishi kuwatetea wanyama na kuwasahau wanadamu,la hasha. Ninachokitetea na uwepo wa win-win situation kwa sisi wanadamu na kwa wanyamapori. Kwani kila upande unategemea upande mwingine kwa kiwango kikubwa. Wanyamapori wanatupa mapato na aesthetic values. Nao wanatutegemea sisi kwa survival yao kwa njia ya kuwatunya na kuwajali.
Hivyo ni vyema kufikiria pande zote.