Wito kwa JK: Jenga Serengeti Highway na Fast speed Rail


Mkuu barabara iliyopendekezwa kujengwa pale Serengeti ina madhara makubwa sana katika ikolojia na ikosistimu ya Serengeti-Masai Mara. Pale pana Ushorobo (wildlife corridor) ambayo inatumika wakati wa Nyumbu, Pundamilia na wanyamapori wengine wanapoenda Masai Mara wakati wa kiangazi Serengeti na wanaporudi Serengeti, pale panapokua na kiangazi Masai Mara. Hivyo kujengwa kwa barabara katika eneo lilipendekezwa kusingekua na faida yoyote kwa taifa na pia wanyamapori. Kwani kuvurugwa kwa ikolojia hiyo kungesababisha wanyamapori wengi kufa pale majira yanapobadilika. Au pia ingeweza kusababisha wanyamapori hao kuongeza muingiliano wao na binadamu, kwani wangeweza pia kuvamia maeneo ya binadamu katika kutafuta malisho.
Nafikiri watu wengi hawafahamu kwa undani suala hili. Kwa manufaa endelevu kwa taifa kiujumla, imependekezwa ijengwe barabara kwa route nyingine, tena yenye manufaa makubwa kiuchumi kuliko hiyo ya kupitia Loliondo.

Angalia link hii chini kwa reference na information zaidi.

http://www.savetheserengeti.org/wp-content/uploads/2010/06/Connecting_Northern_Tanzania_FZS_1.pdf
http://www.savetheserengeti.org/wp-content/uploads/2010/06/Serengeti_map.jpg

Pale Tsavo hiyo railway na roadway hazina madhara makubwa katika ecosystem na ecology ya Tsavo kama ujenzi wa Serengeti ungekuwa katika ecosystem ya Serengeti-Masai Mara. Kwanza umaarufu wa Tsavo unatokana na uwepo wa tembo kwa kiwango kikubwa uwepo wa barabara na reli hakujawaathiri sana zaidi ya ujangili unavyowaathiri. Tofauti na Serengeti ambapo Nyumbu kwa kiwango kikubwa wanachangia uimara na uwepo wa stable ecosystem katika mbuga hiyo. Hivyo kuathiriwa kwa wanyamapori hao kutaleta athari katika ecosystem nzima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…