VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Natoa wito wenye mvuto. Kwa makada wenzangu wa CCM na wakereketwa wa chama na wananchi wote kwa ujumla wanaokiunga mkono Chama cha Mapinduzi. Wito wa kuwaomba, kuwashawishi na 'kuwalazimisha' Wagombea wetu hasa wa Urais na Ubunge waitake na kushiriki kwenye Midahalo ili kupima uwezo wao. Uwezo wa kujieleza, kujieneza, kujinyenyekeza, kujitweza bila kubeza na hoja kuzijibu mujarabu kama jawabu.
Hatuna haja ya kuogopa. Hatuna haja ya kukwepa kama kuruka pipa. Hatuna haja ya kuona tunaonewa au wagombea wetu kushambuliwa na kuchambuliwa. Wagombea wetu tunawaamini. Wagombea wetu wako vyema kama vema kwenye daftari la Neema. Wagombea wetu wanajua mambo. Tuna wasomi na wanasiasa wabobezi kwenye wagombea. Hofu yetu inatoka wapi? Midahalo ni muhimu. Ni uwanja wa kuonesha umwamba wa hoja za haja na mipango yenye viwango.
Tuwaache wagombea wetu waitake, waisake na washiriki kwenye midahalo. Hakuna haja ya Katambi, Mwakibinda au Mchange kuingia kati kama nati na kutaka kuharibu ladha ya uchaguzi. Kwa kutaka wao ndiyo washiriki Midahalo. Wao washiriki kama akina nani chamani na uchaguzini? Waachwe wagombea waoneshane ubabe kabla ya kwenye debe la kura. Waziseme sera; waoneshe dira bila hila na kuteka hadhira.
Midahalo ni muhimu. Mbona Hayati Benjamini William Mkapa alishiriki na kufunika?
Mzee Tupatupa wa Lumumba(kwa sasa jijini Dodoma).