Wito kwa nchi zinazotegemea misaada kutoka nchi za Magharibi kusitisha kwa muda na kupitia mikataba yote ya rasimali zake na makampuni yao

Wito kwa nchi zinazotegemea misaada kutoka nchi za Magharibi kusitisha kwa muda na kupitia mikataba yote ya rasimali zake na makampuni yao

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Salam wanajamvi,

Moja kwa moja kwenye mada naomba tuunge mkono hoja hii ya kutaka serikali yetu kua kinara nchi ambazo zitasitisha shughuli zote za miradi ya maliasili na kupitia upya mikataba hio endapo inaendana na maslahi ya sasa.

WITO huu unatokana na juhudi kubwa za usitishaji kwa muda kwa ajili ya uhakiki wa MISAADA wanayoitoa katika nchi zetu. Hivyo nasi kama viongozi timamu na akili ya kawaida hatunabudi kujifunza katika hili kwa ajili ya maslahi mapana kwa NCHI yetu.

Zoezi hilo litaboresha mahusiano na kufanya wakuheshimiana kwakua na faida yenye uwiano.

Zoezi hili pia litawapunguza utegemezi kwa mataifa ya MAGHARIBI na kupunguza mashaka ya ufisadi na matumizi mabaya ya Kodi zao.

Naomba salamu hizi zimfikie Mh. Rais mama yetu shupavu na jasiri, mama ambaye alijitabanisha kua hapangiwi na mataifa ya MAGHARIBI, tuna mwomba atusaidie katika hili ili abaki katika historia ya taifa hili milele na milele.

Ahsante
 
Back
Top Bottom