Wito kwa Rais Magufuli, tuletee Muungano wa Serikali Moja

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Wajumbe,

Nianze kwa kukumbushia andiko langu juu ya hatari iliyopo kwenye muundo wa muungano wetu hususan katika zama hizi za vyama vingi.

Kwakua kupitia uchaguzi wa 2020 chama cha mapinduzi kimeshika hatamu bara na visiwani, hii ni fursa adhimu ya kuyatibu magonjwa yote yanayo usumbua muungano wetu.

Hivyo kwa moyo wa kizalendo kabisa, nitoe wito kwa mwenyekiti wetu na rais wa JMT, mheshimiwa sana Dr. Magufuli J.J.P, anzisha mchakato kutokea ndani ya chama, ili tuweze kufanya mabadiliko ya katiba yetu na kuleta muungano wa serikali moja.

Faida za serikali moja ni nyingi mno, kuanzia na kuimarisha umoja wa kitaifa, kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa n.k.

Uchaguzi wa 2025 uwe ni wa kuchagua serikali moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia ikikupendeza, 2025 tuletee mheshimiwa Mwinyi awe Rais wa kwanza kufungua kurasa za JMT mpya.
 
Umejuaje kwamba huwa anapita???

Badala ashughulike na SGR, kupanda kwa bei ya sukari, mafuta ya kula, cenent nk, apoteze muda wa kupita humu??!!
Kazi na dawa, mheshimiwa ni mzuri sana kwenye 'multitasking'. Pia ni msikivu, ni lazima ajue watu wake wana maoni gani.

Na hata ikitokea yuko busy, basi wapo watu wanaokusanya taarifa na kuzichakata, kisha wanazitumia kumshauri rais na serikali yake.
 
Itakuwa huna taarifa,hivi sasa tulipo kila mmoja na nchi yake kilichopo kinaitwa kwa lugha ya kitaalamu mazingaombwe.
 
Hakuna kitu hicho kwa serikali hii, sio wasikivu, wanasema ni wasikivu na wanyenyekevu kipindi cha kuomba kura tu.
 
Naunga mkono hoja yako ila kushinda uchaguzi sio tatizo, kwanza uje uchaguzi wa kuulizwa wananchi kama muungano wanautaka au hawautaki , Lkn sio tume hizi za uchaguzi, kama wananchi tutachagua wa kusimamia hilo zoezi.
emoji1317.png
 
Unajua siku hizi WaZanzibari hawana habari na serikali ya Tanganyika au Tanzania bara kama tulivyozoea ,wala huwasikii kuitajataja.
 
Kwa muda mrefu uchumi wa nchi hii umekuwa ukihudumia siasa,na nchi imeendelea kuwa maskini.

Sasa hv tunachotaka, ni kazi kwenda mbele,sio kazi za kimachinga, za kuuza leso na miwani kutoka china,
Tunahitaji mapinduzi ya viwanda.

Miradi yote ya ujenzi wa Miundombinu inabidi ijengwe na sekta binafsi chini ya uangslizi wa serikali,ikibidi wakandarasi wakusanywe wafanye kazi kwa pamoja.

Niliuliza kwanini hatuzalishi sukari na mafuta ya kula ya kutosha,nikaambiwa sio kwa sababu hatuwezi au hatuna tekinolojia,shida Kuna watu wanakula kupitia hiyo nakisi,na hawataki iondoke sasa vitu Kama hv,Ili tuendelee inabidi tuachane navyo. Na mambo ya umungu mtu,tuyaache

Uwezi kuchukua 1.5Tilioni,ukaenda kujenga uwanja wa Ndege kwenye mji mdogo Kama Chato,au,songwe,au Masasi,ukaacha Miji mikubwa Kama Mbeya,Mwanza,Arusha,
 
Itakuwa huna taarifa,hivi sasa tulipo kila mmoja na nchi yake kilichopo kinaitwa kwa lugha ya kitaalamu mazingaombwe.
Hicho ndicho tunataka kukiondoa. Utanganyika na Uzanzibari ufe, ubaki utanzania.
 
Unajua siku hizi WaZanzibari hawana habari na serikali ya Tanganyika au Tanzania bara kama tulivyozoea ,wala huwasikii kuitajataja.
Wameiimarisha sana SMZ, ni jambo la hatari kwa muungano.
 
Naunga mkono hoja yako ila kushinda uchaguzi sio tatizo, kwanza uje uchaguzi wa kuulizwa wananchi kama muungano wanautaka au hawautaki , Lkn sio tume hizi za uchaguzi, kama wananchi tutachagua wa kusimamia hilo zoezi [emoji1317][emoji4]
Mkuu wakati wa kuungana hatukuulizwa, hakuna haja ya kutuuliza tena. Wawakilishi wa wananchi wafanye kazi yao.
 
Kazi na dawa, mheshimiwa ni mzuri sana kwenye 'multitasking'. Pia ni msikivu, ni lazima ajue watu wake wana maoni gani.

Na hata ikitokea yuko busy, basi wapo watu wanaokusanya taarifa na kuzichakata, kisha wanazitumia kumshauri rais na serikali yake.
Hapa unaongelea Rais wa Burma.
 
Kwa muda mrefu uchumi wa nchi hii umekuwa ukihudumia siasa,na nchi imeendelea kuwa maskini.
Sasa hv tunachotaka, ni kazi kwenda mbele,sio kazi za kimachinga, za kuuza leso na miwani kutoka china,
Tunahitaji mapinduzi ya viwanda,
Miradi yote ya ujenzi wa Miundombinu inabidi ijengwe na sekta binafsi chini ya uangslizi wa serikali,ikibidi wakandarasi wakusanywe wafanye kazi kwa pamoja.
Niliuliza kwanini hatuzalishi sukari na mafuta ya kula ya kutosha,nikaambiwa sio kwa sababu hatuwezi au hatuna tekinolojia,shida Kuna watu wanakula kupitia hiyo nakisi,na hawataki iondoke sasa vitu Kama hv,Ili tuendelee inabidi tuachane navyo,
Na mambo ya umungu mtu,tuyaache,
Uwezi kuchukua 1.5Tilioni,ukaenda kujenga uwanja wa Ndege kwenye mji mdogo Kama Chato,au,songwe,au Masasi,ukaacha Miji mikubwa Kama Mbeya,Mwanza,Arusha,
Hili limenipitia mbali, kumbe 1.5 trillions zimejenga viwanja vidogo na miji kama Mwanza, Arusha na Mbeya hakuna Airports. Ni kitu kibaya.

Hizi Airports kubwa za Songwe, Mwanza na Arusha Airports zipo miji gani? Na zote hizi ni ndogo sana kuliko Chato?
 
Wajumbe,

Nianze kwa kukumbushia andiko langu juu ya hatari iliyopo kwenye muundo wa muungano wetu hususan katika zama hizi za vyama vingi.

Kwakua kupitia uchaguzi wa 2020 chama cha mapinduzi kimeshika hatamu bara na visiwani, hii ni fursa adhimu ya kuyatibu magonjwa yote yanayo usumbua muungano wetu.

Hivyo kwa moyo wa kizalendo kabisa, nitoe wito kwa mwenyekiti wetu na rais wa JMT, mheshimiwa sana Dr. Magufuli J.J.P, anzisha mchakato kutokea ndani ya chama, ili tuweze kufanya mabadiliko ya katiba yetu na kuleta muungano wa serikali moja.

Faida za serikali moja ni nyingi mno, kuanzia na kuimarisha umoja wa kitaifa, kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa n.k.

Uchaguzi wa 2025 uwe ni wa kuchagua serikali moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia ikikupendeza, 2025 tuletee mheshimiwa Mwinyi awe Rais wa kwanza kufungua kurasa za JMT mpya.

Ni kweli ccm wako wengi kwenye mabunge yote, je wingi wao huko bungeni unatokana na ridhaa ya kweli ya wananchi walio wengi? Ukitaka kuunganisha nchi lazima uwe upo madarakani kwa ridhaa ya walio wengi.
 
Wajumbe,

Nianze kwa kukumbushia andiko langu juu ya hatari iliyopo kwenye muundo wa muungano wetu hususan katika zama hizi za vyama vingi.

Kwakua kupitia uchaguzi wa 2020 chama cha mapinduzi kimeshika hatamu bara na visiwani, hii ni fursa adhimu ya kuyatibu magonjwa yote yanayo usumbua muungano wetu.

Hivyo kwa moyo wa kizalendo kabisa, nitoe wito kwa mwenyekiti wetu na rais wa JMT, mheshimiwa sana Dr. Magufuli J.J.P, anzisha mchakato kutokea ndani ya chama, ili tuweze kufanya mabadiliko ya katiba yetu na kuleta muungano wa serikali moja.

Faida za serikali moja ni nyingi mno, kuanzia na kuimarisha umoja wa kitaifa, kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa n.k.

Uchaguzi wa 2025 uwe ni wa kuchagua serikali moja ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia ikikupendeza, 2025 tuletee mheshimiwa Mwinyi awe Rais wa kwanza kufungua kurasa za JMT mpya.
Hio serekali moja mwambie akupelekee kwa mkeo Bladibasketbol Instabul bangaladdesh ww
 
Back
Top Bottom