nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,285
- 3,250
..Mosi...Hongera kwa walioteuliwa kwenye bunge la katiba .....hata kama ni kwa kulipana fadhila..
..Pili..nategemea mtamchagua mtu makini asiye na doa kiutendaji kuwa mwenyekiti wenu wa kudumu ...sitegemei mchague fisadi liwe mwenyekiti wenu .....maana tumechoka nchi hii kuona mafisadi wakifanya watakavyo bila kuchukuliwa hatua na watawala..Sasa nyie wajumbe nategemea hamtafanya kosa hilo...
...Tatu..wakati mtakapoanza mjadala wa katiba proper ni mategemeo yangu kuwa mtakua mnatafakari majanga yafuatayo kwenye utawala huu....ili liwe kama angalizo kwa maamuzi yenu mkiwa Dodoma kwa hizo siku 70(ama 90)...
..Ndugu zangu haya kama si majanga kwenye utawala huu ni nini??...hakuna utawala tumewahi kuwa nao wenye majanga kama haya...aniambie mtu humu...Kinachosikitisha haya yote yanatokea lakini mambo ni "business as usual"..
..WITO KWENU (kama way forward).....
...Pamoja na kwamba wengi mmepeana mikakati ya kujadili muundo wa muungano na serikali zake...mi bado naona tatizo kubwa la taifa letu limekuzwa zaidi na namna viongozi wetu wanavotutawala kuliko aina ya muundo wa muungano(serikali)..Nasema hivi nikiwa na maana kwamba hata mje na muundo bora namna gani...lakini kama viongozi wetu(rais)watakuwa hovyo basi hata manufaa ya muundo mzuri wa muungano (serikali)hayataonekana....Kwa maana hiyo lazima mjadili jinsi nzuri ya kuwadhibiti wale tunaowapa dhamana ya kutuongoza kama nchi...Hii itasaidia kuondoa nepotism ambayo imekithiri kwenye taifa hili ......maana rais anapokuwa bogus watu wake wanavurunda tu huku wakijua hawatadhibitiwa...hili lazima mlifanyie kazi....
....tafakari....msihadaike na posho za kukaa....chukueni hatua....

- Ni kwenye utawala huu ubora wa elimu umeshuka kwa kiwango cha kutisha...kiasi cha kuamua kushusha madaraja ya ufaulu kwa wanafunzi....
- Ni kwenye utawala huu biashara ya madawa ya kulevya imekithiri kiasi cha kuathiri sifa ya nchi hii..
- Ni kwenye utawala huu tembo wetu wameuwawa na karibia wanamalizwa...na wahusika wanapeta mitahani huku wakila maisha..
- Ni kwenye utawala huu raia wameuwawa na kuteswa na makanisa kupigwa mabomu na kuchomwa kwa jinsi ambayo haijawahi kutokea kwa taifa hili..
- Ni kwenye utawala huu deni la taifa limeongezeka kwa kiwango cha kutisha (tunaambiwa ni zaidi ya trillion 27).....deni hili litakuja kulipwa na wajukuu zenu...
- Ni kwenye utawala huu watu wanaona ufahari kuiba pesa za umma maana hawachukuliwi hatua...
- Nchi hii pamoja na utajiri mkubwa wa asili lakini bado inategemea nchi wahisani ili isonge mbele...na hata bajeti zake kila mwaka zinakuwa na nakisi (budget deficit)..tujiulize hela za madini....utalii...misitu...gas n.k zinakwenda wapi???....
..Ndugu zangu haya kama si majanga kwenye utawala huu ni nini??...hakuna utawala tumewahi kuwa nao wenye majanga kama haya...aniambie mtu humu...Kinachosikitisha haya yote yanatokea lakini mambo ni "business as usual"..
..WITO KWENU (kama way forward).....
- Lazima katiba mpya ije na suluhisho la baadhi ya majanga haya...kama uwezekano wa kumwondolea rais kinga ya urais (presidential immunity)mara amalizapo mda wake wa urais....ili aogope kutumia madaraka yake vibaya akijua ataadhibiwa na sheria za nchi mara atakapotumia madaraka yake vibaya.....
- Pia katiba mpya lazima iangalie namna ya kudhibiti rais asifanye "nepotism" (uswahiba) akiwa madarakani....kwa maana ya kudhibiti teuzi za rais katika ngazi zote ili asilundike washkaji madarakani kiasi cha kushindwa kuwachukulia hatua pale wanapovurunda...kama tulivyoona sana kwenye utawala huu...Lazima katiba mpya ije na proper vetting mechanisms za teuzi za rais.....hata kule marekani rais anateua lakini lazima watu wawe scrutinized kwenye senate na congress kabla ya kukubaliwa.....
- Pia suala la rais kufanya biashara akiwa madarakani lazima litazame kwa kina katika mijadala ya rasimu ya katiba mpya...tumeshaona marais wakitumia ikulu yetu kufanikisha biashara za family zao...mifano ipo....wapo hata wake wa marais wameanzisha taasisi binafsi wakiwa ikulu...na wanapoondoka madarakani wanaondoka nazo...Wapo pia watoto wa marais waliopata utajiri wa kutisha mda mfupi tu baada ya wazazi wao kuwa marais....wakati walikuwa watu wa kawaida tu kabla ya hapo....
- Lazima katiba mpya imdhibiti rais kama twataka kutoka katika mgando huu....maana rais akiwa effective hata mifumo mingine ya kiutawala itakuwa effective....Lakini rais akiwa bogus kwasababu tu katiba haimbani mambo hayataenda....tumeshaliona sana hili.....