Wito kwa Wana-JF wote

Yaani kuna mambo yanachekesha kama sio kukera.Inawezekana huko nyuma kuna mtu alikuja na proposal kama hii.Lakini hiyo haiondoi umuhimu wa kukumbushana especially kutokana na ukweli kwamba so far hakuna hatua zilizokwishachuliwa.

Utasikia watu wanasisitiza kilimo,leta majembe waende shambani,wanaanza excuse ...nilianza proposal yangu kwa kubainisha wazi kwamba ninachoandika sio sign ya ku-resign ktk haya mapambano bali kukumbushana wajibu wetu.Kinachofanyika JF ni cha muhimu na ni lazima kiendelee:to unearth the evils in our society.However,we could well move beyond that.

Sio suala la ndivyo tulivyo au sivyo tulivyo,kwa vile misaada inatolewa sehemu mbalimbali duniani (in fact hata US ilipewa misaada wakati wa Katrina),na misaada ni silaha,that's how ECONOMIC SANCTIONS works kwa walio wagumu kutafsiri mambo.Pengine JUST WAR THEORY inaweza kutoa mwanga wa effectiveness au immorality ya actions zinazoweza kuwa na madhara limited but faida za kutosha in the long run.
 
we peasant nini?? kuna subway dizim wewe!!! na vi-shop flani flani vinauza burgers na pizza, wao wanadhani ndio ujiko........matozi tauni pale wakiwa na dates wanaenda kutia nazo msosi subway!!! kwikwikwikwikwikwikwi, kaaaaaaazi kweli kweli.

Steers na Nandos...ebanae inanikumbusha enzi hizo lazima matozi waende Fosters.
 
icadon,
yap, mambo ya upstairs!! dizaini Nyani, Dar ilikuwa EXIT nini!!???

mlalahoi, mie naona soln ni hiyo tu kupiga debe misaada isitishwe!! 'till then labda hawa walafi wetu watatia akili.
 
Bongo junk foods zitoke wapi bana...wewe umewahi kuona Wendy's au Quiznos bongo..?

junk food sio lazima ziwe quiznos wendys, micky d, burger king... hizo ni brand names tu, junk food hata nyumbani kwako unaweza kutengeneza ! chipsi dume, na vingine viiiingi pia vinaweza kuwa home made na vikawa junk vile vile !
 
haa ahaha ahaha ahaha..sound like you aint been there lately.

Nyie vipi nyinyi...mwenzenu nilikuwa natania tu haina maana sijarudi bongo muda mrefu. Nilikuwepo huko juzi juzi tu hapana sikuona lolote la maana linaloendelea zaidi ya mivumbi tu...
 
Nyie vipi nyinyi...mwenzenu nilikuwa natania tu haina maana sijarudi bongo muda mrefu. Nilikuwepo huko juzi juzi tu hapana sikuona lolote la maana linaloendelea zaidi ya mivumbi tu...

usifikiri ukadhani.....
 
Miaka 30 iliyopita Tanzania imepokea misaada ya karibu dola bilioni mbili. Ndani ya miaka kumi iliyopita kwenye taasisi moja (Benki Kuu) tumepoteza Dola Bilioni moja (ukiunganisha na hizo za EPA) - Kumbeni Rais alisema hizo zilizopotea si fedha za wafadhili bali ni za... . Kila mwaka kwenye halmashauri, wizara, wakala na taasisi huru za serikali tunapoteza shilingi karibu bilioni 300? kwa matumizi mabaya, wizi n.k

Sasa mnijibie maswali mawili kama siyo matatu ninyi ambao mnashtuka kuona misaada inasitishwa kana kwamba ni "stupid idea".

- Je Tanzania inahitaji misaada kutoka nje ili iweze kujenga hospitali, shule, barabara, n.k ?

- Je, Tanzania ikiweza kusimamia fedha zake vizuri yaweza kupunguza utegemezi wa wafadhili hata kununua chandarua milioni tano?

- Je, misaada kukatisha ni suala baya sana kwa Taifa?
-
 

Mimi sio mmojawapo ninayeshtuka kuona misaada inasitishwa bali napinga hii dhana ya kupewa misaada kila siku huku bado tukiwa masikini wa kutupwa. Mimi nasema tunaweza kufanya vitu vingi sisi wenyewe.

Tanzania haihitaji fedha kutoka nje kujenga hospitali, shule, wala barabara.

Ndiyo, Tanzania inaweza kabisa kusimamia fedha zake vizuri na kuondoa kabisa utegemezi wa wafadhili. Kama Lowassa aliweza kusaidia kuchangisha milioni 400 katika siku mbili tatu za kuipongeza Taifa Stars kwenye kaushindi kadogo kasiko hata na maana yoyote kwa nini serikali ishindwe kupata/ kuwa na hela za kutosha kuendesha miradi ya maendeleo? Hili linawezekana kabisa ila basi tu....labda kwa vile.....

Actually misaada kusitishwa itakuwa ni jambo zuri kutokea Tanzania tangu uhuru! Usitishwaji utatufanya tuwe resourceful in harnessing our natural resources to gain the economic growth we desire. Misaada hii kwa kweli imetulemaza kiasi kwamba tunaona hatujiwezi bila ya wao na ndio maana unaona baadhi ya watu humu wakinung'unika juu ya vitisho vya usitishwaji huo.

Kwa hiyo mimi nasema waache tu kutupa hiyo misaada tutajiju!!!
 
Mnyika kanenepa siku hizi? dizaini naye keshakuwa fisadi...

Mkuu anafanya mazoezi kwa ajili ya 2010, si unajua usipokuwa baunza wazee wanaitumia kama silaa ya kukumaliza?

Kwa mfano wanaweza kusema ni mtoto, bado hajashiba nk..

Hayo yote yanaweza kukfanya usifanikiwe
 
...................


1. Vyama vya Upinzani vilivyo serious viandae maandamano ya kutosha juu ya Kupinga Ufisad ktk Nchi yetu, kwani hadi sasa Bunge halijatoa adhabu maalum kwa wanaolifilisi TAIFA.
Tuwape muda upinzani uandae hio...


tSiyo tu waandamane, bali pia sasa ni wakati mwafaka wa kushinikiza mabadiliko ya katiba inayokidhi mfumo unaoendana na vyama vyingi. Na kwa waziri wa fedha kujikanyaga kwamba mafisadi wamerudisha pasa za EPA lakini kutajwa ni akina nani au kampuni zipi ni dalili ya kuwa ufisadi bado unakumbatiwa, hivyo vyama vya upinzani vingeshikia kidedea hili kupleka hoja hizi kwa wananchi na serikali nafkiri itatoka usingizini.
 
Ukiangalia hoja mama, watu wengi wamejitahidi kuchangia lakiniw apo waliokwenda nje kabisa ya hoja hiyo. Lakini hiyo inatoakana na mwelekeo wa michango inayotolewa. Si vibaya. Sasa naomba turudi kwenye hoja ya msingi, tutoe maoni kuhusu lililopendekezwa kwa sababu kitakachofanyika kinaweza kuwa mchango mkubwa wa JF katika action inayotakiwa kurekebisha hali ya mambo nchini.
 

MKJJ,

Kula 5! 40 years sasa baada ya uhuru and we are heavily dependent on aid.. yaani hand outs?????? Watz tuone aibu!

Hivi mnajua TRA hukusanya tu 14% ya kodi Tz?

Hatukitaji misaada..na hii Umatonya ndo imetudumaza hata akili kutokuwa innovative na kuwakamata mafisadi na kukosa uadilifu!

Je misaada ni msingi wa maendeleo?
 



Ni kweli.

Hebu Fikiria Bush kaja juzi hapo Dar katoa $700kasoro Million, watu wamekenua meno na kutabasamu kama Bunny.

Kwa nini watanzania hao hao wanashindwa kushangaa ni vipi tunafurahia hizo chache za misaada wakati tumeibiwa $ Billion kutoka kwenye aacount moja tu?

Ni ulemavu wa akili kushangilia misaada na kuwaachia wakoloni wa ndani waishie na mabillioni.
Tena kuna wengine hapa wana mawazo ya kasorobo, kwamba hata zisingeibiwa mimi au wewe tusingezipata.

Kuna mamabo mengi ambayo ni utajiri wa pamoja hata kama jioni utajiri huo huwezi kurudi nao nyumbani.

Mbuga ya serebgeti ni yetu wote, ni mjinga tu anayedhani wanyama wote wakiuzwa kwa waarabu wa Saudia yeye hana cha kupteza.

Mlima Kilimanjaro ni wetu wote sisi wa malinyi na wale wa Sanya juu. Ni ujinga kudhani mlima huo ni fahari ya wamachame tu na sisi Wabenamanga tuendelee kula pepeta tu.

Tuna fedha nyingi kutoka kila kona ya nchi lakini kibaya ni kwamba Chama kinacho tawala bado kina msimamo kama vile nchi imepata Uhuru jana. SISIEMU bado kiko kwenye hali ile ya chama kilichokwisha twaa Uhuru kutoka kwa wakoloni sasa hakijui nini cha kufanya.

Hiyo misaada yote isitishwe aua igeuzwe katika namna ambayo haitatupa ulemavu, kama vile misaada iwe ni ya kusomesha watu tu.
Lakini kwa nchi ya Mafisadi kama yetu utashangaa watao enda kusoma huko ni Wasomali Wahindi toka India, Warundi na Wakenya na kidogo watoto wa Mafisadi, ambao wengi wakija hapa wanajifunza kuvuta yale mabaki ya Kokaini.

lakini kikubwa zaidi ni sisi wenye mawazo mapay kujitokeza kugombea nafasi za ubunge ili tukomeshe hali hiii tegemezi.
 
Wana JF ambao wanaona hizi ni kelele tu nawashangaa sana. Hivi hamjui ya kuwa mafisadi waliotajwa sasa wameweka ntitedi vioo vya magari yao kwa ajili ya woga wa kuzomewa na wananchi wakipita barabarani. Hizi sio kelele, mafisadi sasa wanajificha hawana raha ya kujichanganya kama walivyozoea, kama unafikiri hizi ni kelele fikiri tena. Watoto wa muheshimiwa fulani walikimbia supermarket kutokana na watu kuwazomea kuwa mafisadi, walipoana kila wanakokwenda wanazomewa walitimua mbio kurudi kwenye nyumba yao ya ufisadi, Hizi sio kelele raha hawana, tunasubiri siku tutakayo kataa zaka yao kanisani.
 

Wakati mwingine sie wahanga wa ufisadi ni sehemu ya tatizo kwa vile pale tunapopaswa kuongea kwa vitendo sie tunaendelea kuongea kwa maneno.Tunapiga politiki.Nakubaliana nawe kwa asilimia 100,Mpita Njia,kwamba kinachohitajika hapa ni NINI kifanyike.Let's go back to hoja mama.
 
STUPID IDEA ! unadhani tz kama taifa kunyimwa misaada itawaathiri akina nani kama sio innocent poor people !.... are we using our own circle of darkeness to light up the room ?

We Kada, Usitake kutubabaisha na hoja zako zinazotetea makombo unayorushiwa na hawa maafisadi. Tangu lini Watanzania wanafaidika na pesa hizo za misaada kama sio hao baba zako tu?
Hizo pesa zilizokuwa kwenye mfuko wa EPA,toka UK,Japani zimemsaidia Mtanzania yupi wewe unayetaka tuamini? Pesa za msaada toka UK wakanunulia Radar na Ndege,haviwasaidii watanzania hivyo,Pesa toka Japani wamekula Mkapa,Mramba na hao Magabachori.Hebu tuambie zimewasidia vipi watanzania zaidi ya kuwasaidia hao Mabwanyenye wako. Wewe kweli ungekuwa na huruma na Watanzania usingekuwa unakuja humu kukejeli juhudi mbalimbali za Wazalendo.

Hivyo basi wazo lililotolewa ni zuri na hakuna watakachopoteza watanzania kwani walikuwa hawakipati toka mwanzo kutokana na misaada hiyo.
 
JAMANI HUMU KUNA MAFISADI WAHISANI WAAMBIWE,WATU WA DINI ZOTE MPAKA WATOTO KWANINI SISI TUMEKOSA NINI MPKA TUTESEKE WAKATI HII NCHI WALIO IPIGANIA HAWAPO SO KAMA NI KUGAWANA WOTE NI PASUPASU.MOTO UWE ULEULE.HAPOZWI MTU HUMU.
 
.....hivi hapa ni muafaka gani umefikiwa?? au ilikuwa ni thread tu ya kuongeza namba za thread?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…