.....hivi hapa ni muafaka gani umefikiwa?? au ilikuwa ni thread tu ya kuongeza namba za thread?
Hivyo basi wazo lililotolewa ni zuri na hakuna watakachopoteza watanzania kwani walikuwa hawakipati toka mwanzo kutokana na misaada hiyo.
Ndio tatizo hilo,Mkuu.Kuna wenzetu priorities zao ni wingi wa posts bila kujali contents za wanacho-post.That's why inakuwa vigumu kufikia conclusions kwenye baadhi ya hoja au mada.Hebu angalia ile ya madai kuhusu kufeli kwa Mbowe inavyozidi kuwa ndefu ilhali kinachoongelewa humo ni more than questionable.Anyway,tunawapigia kelele wanasiasa kwa kuendekeza maneno mengi bila vitendo wakati sie wenyewe tunakuwa wazito kufanya kinyume cha hivyo.Ndio JF hiyo!
Swala la kunyimwa misaada mi nadhani na ninaamini kabisa halitatuathiri sisi wananchi. Litawaathiri wakina Chenge na mafisadi wenzake. Maana ki ukweli hata hiyo 50% ya bajeti ambayo tunauwezo nayo kama ingekuwa inatumika vyema kwa maslahi ya wananchi tungekuwa na hali nzuri zaidi ya hapa tulipo. So swala la misaada ni zero kabisa. Halina maslahi kwetu sisi wananchi walio wengi (ukiacha wananchi wa masaki na Oysterbay) Hata wangekaa na hela zao hao wazungu waathirika ni mafisadi na familia zao wanazozigharimia huko nje na hapa nyumbani kwa migongo yetu.
Hoja ya Mlalahoi nadhani ina mantiki kubwa sana. Maoni yangu: Cha kufanya hapa ni kutumia hizo evidence kwa mfano za mikataba fake tukaanza kuzipublicize kwa hizi global media na think tanks. Infact siku hizi kuna wanaharakati ambao wana influence kweli kweli kwenye serikali zao, cha kufanya ni kuwasukumia hii mikataba ya kifisadi na in the process wataifikisha kwa wanasiasa wao. Na uzuri wanasiasa wa huko majuu wanasoma documents, sio kama wa kwetu.
Kwa hiyo wito wangu, watu waendelee kuanika hii mikataba na haya madudu hapa na wale wenye uwezo waanze kuisukama sehemu mbali mbali. Atleast tukianza na "name and shame" haitakuwa mbaya katika global level watu wakajua wanadeal na viongozi wa namna gani.
Kingine tunaweza kutumia hii mikataba ku-lobby especially kama huko USA watu wakaanza na members wa congress. It is possible.
Kwa hiyo Mlalahoi hoja yako ni very valid kabisa na walio wengi hapa naamini wanaiunga mkono. We cant defeat mafisadi by reasoning and writing only, neither can we defeat them without the two. So we should know that this is a very long and dangerous battle because you are stepping on people`s toes..but again its the only way.
Apologetics wasitake kutumia mgongo wa walalahoi..kutetea ufisadi...eti wahisani wakisitisha misaada wananchi wataumia? Wananchi gani hao???????? Kwani kwa kidogo tulicho nacho kama kingetumika vyema kwa maslahi ya wote..tungekuwa na hali nzuri zaidi kuliko sasa hivi! So misaada haina maana kwetu sisi walalahoi!