Doctor Mama Amon
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 2,089
- 2,725
Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Afya, na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, Tanzania
I. Usuli
Kwa mujibu wa Dokezo la Kisera (Policy Brief) linalojadiliwa hapa, ninyi Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, na Mkrugenzi Mkuu NHIF, Irene Kisaka, mnakumbushwa kutekeleza majukumu yenu vizuri zaidi kwa kutatua tatizo lifuatalo mara moja, kabla ya kushughulikia matatizo mengine yoyote:
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, yaani NHIF, Bado Unafanya Kazi Kiswahili Badala ya kufanya kazi kwa Kuzingatia “Service Delivery Cycle” inayowawezesha wananchi kupata huduma bora za bima ya tiba kwa wakati na zilizo karibu na makazi yao.
II. Utangulizi
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unabeba dhima ya kupanua huduma za tiba kwa njia ya upatikanji wa huduma za matibabu kwa bima, badala ya matibabu kwa fedha taslimu.
Ni hatua muhimu kuelekea maono ya bima ya afya kwa wote nchini Tanzania.
Lakini, kasi ya utendaji wa kazi za NHIF kwa sasa inaashiria kwamba ndoto hii haitafikiwa kama hatua za mageuzi ya kifikra na kitabia hayatafanyika mara moja.
Aya zifuatazo zinaweka bayana urefu na upana wa tatizo hili.
Kwa mujibu wa Kanuni za sasa, mfuko wa NHIF unapaswa kutoa huduma kwa kuzingatia “service delivery cycle” yenye hatua 12, tangu maombi yanapofanywa na kituo mpaka malipo ya kwanza yanapofanywa na NHIF Kwenda kwa kituo, kama mchoro ufuatao unavyoonyesha:
Chanzo: Mwandishi
Ufafanuzi wa “service delivery cycle” kwa kutumia maneno ni kama ifuatavyo:
- MOSI, mmiliki wa kituo kutuma maombi rasmi ya kutoa huduma za afya kwa wanachama wa NHIF kupitia mlango maalum wa kimtandao (NHIF online portal).
- PILI, Kamati ya Mkoa ya NHIF kupokea na kuhakiki maombi na kuandaa taarifa ya mapendekezo kwenda kwenye Sekretarieti ya Makao Makuu.
- TATU, Sekretarieti ya Makao Makuu, kupokea maombi na kuyasukuma kwenye Kamati za kusimamia uzingatiwaji wa sheria za nchi (legal and anti-fraud units) kwa ajili ya uhakiki.
- NNE, Kamati za kusimamia uzingatiwaji wa sheria za nchi (legal and anti-fraud units) kuhahakiki maombi haya, na kisha kuandaa taarifa ya mapendekezo kwenda kwenye Sekretarieti ya Makao Makuu.
- TANO, Sekretarieti ya Makao Makuu, kukusanya maombi ya Kituo, taarifa ya Mkoa, Taarifa ya Idara ya Sheria na Taarifa ya Idara ya Kudhibiti Udanganyifu, na kuandaa Kikao cha Kamati ya Wataalam ya Taifa kwa kutumia ajili ya kupokea, kujadili, na kupitisha maombi, kama yatakidhi vigezo. Kamati hii hukutana mara moja kila baada ya miezi mitatu kwa ajili ya kumshauri Mkurugenzi Mkuu.
- SITA, Kamati ya Wataalam kukutana kwa ajili ya kuyapokea, kuyajadili, na kuyapitisha au kuyakataa maombi hayo. Kamati hii inajumuisha wajumbe kutoka Idara ya sheria, idara ua kuzuia udanganyifu, idara ya tiba, na idara baki nyeti. Aidha Kamati hii inayo mamlaka ya Veto dhidi ya Mapendekezo ya ngazi zote za chini.
- SABA, Mkurugenzi Mkuu kupokea taarifa ya mapendekezo ya Kamati ya Wataalam na kuiidhinisha, kama ataridhika na mapendekezo hayo.
- NANE, nakala mbili za rasimu ya mkataba wa mwombaji ulioidhinishwa na Mkurugenzi Mkuu kupelekewa kwa Meneja wa Mkowa wa NHIF.
- TISA, Mwombaji hupata nakala mbili za rasimu ya mkataba ambao haujasainiwa, kupitia kwenye ofisi ya Meneja wa NHIF Mkoa, kuzisaini na kuzirejesha mara moja.
- KUMI, Mkurugenzi wa Tiba, kusaini mkataba wa mwombaji, na hatimaye kupeleka nakala kwa mwombaji kupitia kwa Meneya wa NHIF wa Mkoa.
- KUMI NA MOJA, mwombaji hupokea nakala ya mkataba na kuanza kutoa huduma ya tiba kwa wanachama wa NHIF.
- NA KUMI NA MBILI, Mfuko wa NHIF kufanya malipo ya kwanza kwa mmiliki wa kituo anayetoa huduma kwa wanachama wa NHIF.
Dkt. Irene Kisaka, Mkurugenzi Mpya wa NHIF, Tanzania
III. Tatizo
Ndugu Waziri wa Afya na Mkrugenzi Mkuu NHIF, Pamoja na uzuri wa “service delivery cycle” niliyoitaja hapo juu, kuna changamoto kubwa katika pingili inayoanzia kwenye hatua ya SABA mpaka hatua ya KUMI.
Ni hivi: Mara kadhaa tumeshuhudia Mkurugenzi wa Tiba akisita kusaini maombi ambayo tayari yamepitishwa na Kamati ya Wataalam, na kuidhinishwa na Mkurugenzi Mkuu, wakati Mkurugenzi wa Tiba pia ni mjumbe wa Kamati ya Wataalam inayokuwa imepitisha mapendekezo hayo Kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu.
Na wakati mwingine, kutokana na maoni ya baadhi ya wasaidizi wa Mkurugenzi Mkuu kutoka ngazi za chini, tumeshuhudia Mkurugenzi Mkuu akisita kuidhinisha mapendekezo yaliyopelekwa kwake na Kamati ya Taifa ya Wataalam, wakati maoni kutoka ngazi za chini tayari yanakuwa yamefanyiwa uhakiki katika ngazi ya Sekretarieti, ngazi ya Kamati ya Wataalam, ngazi ya Idara ya Sheria na ngazi ya Idara ya Kuzuia udanganyifu.
Ndugu Waziri wa Afya na Mkrugenzi Mkuu NHIF, Kigugumizo cha aina hii kinapotokea, ukamilishaji wa “service delivery cycle” husimama kwa miezi kadhaa, kwa kuwa mchakato hurudishwa tena kwenye hatua ya tatu ya “service delivery cycle” niliyoitaja hapo juu, badala ya kwenda kwenye hatua ya utekelezaji.
Na jambo hili hutokea bila hata mwombaji kupatiwa taarifa yoyote ili ajue mkwamo uko wapi.
Hata mwombaji anapopiga simu ya ufuatiliaji majibu anayopewa ni “subiri kidogo,” “tuko kwenye mchakato,” “tuko kikaoni,” “hatuwezi kuongea kwa sasa,” tutakukupigia baadaye,” na “Mkurugenzi yuko Dar es Salaam kikazi.”
Na hili la mwisho linakera zaidi maana ni kama vile NHIF hawajui sababu za kukasimisha madaraka.
Sababu ya kwanza ni ukosefu wa muda.
Kwa kuzingatia tofauti kati ya "ofisi" na "ofisa" "ofisa" akisafiri "ofisi" huweza na hupaswa kubakia hai ili utekelezaji wa majukumu husika uendelee kwa njia ya utoaji wa kasma ya madaraka.
Pia ukasimishaji wa madaraka hufanyika pale mwenye ofisi anapokuwa hana weledi stahiki kwa ajili ya kutekeleza kazi fulani.
Kigugumizi cha ukadimishaji wa madaraka maana yake ni kuwa “key business processes” zinazotekelezwa ndani ya NHIF hazijakaa sawa.
Yaani baadhi ya “key business processes” zinaonekana kuwa na mafundo mengi yanayozuia kupatikana kwa matokeo yanayokusudiwa kwa sababu kuna “key business processes jamming.”
Kitaalam tunaweza kusema kwamba ndani ya NHIF kuna “spaghetti-like key business processes.” Jambo hili sio sawa hata kidogo.
Dkt. David Mwenesano, Mkurugenzi wa Tiba na Huduma, NHIF, Tanzania
IV. Mapendekezo
Ndugu Waziri wa Afya na Mkrugenzi Mkuu NHIF, Changamoto hizi zimekuwa zikitokea kabla na baada ya ninyi kuingia kwenye ofisi mnazozikalia kwa sasa.
Lakini, nafikiri kuwa sasa ni wakati wenu wa kuonyesha utofauti kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo.
Zama za giza zilizokuwepo wakati wa Waziri Ummy Mwalimu na Mkurugenzi Mkuu aliyeitwa Dkt. Konga zimepita. Sasa tufungue ukurasa mpya wa uwajibikaji.
Kumbukeni kuwa, mfuko wa NHIF unayo mamlaka ya kusitisha mkataba muda wowote kama utapata taarifa mpya zinazoonyesha kwamba maamuzi ya awali ya kuruhusu kusainiwa na kuanza kutekelezwa kwa mkataba yalitokana na taarifa potofu.
Aidha, and kanuni za utawala bora zinasema kwamba tunapaswa kufanya kazi kwa kufuata “praxiological spiral,” yaani kufanya kazi kwa kufuata mtiririko huu:
“plan, implement, review => plan, implement, review => plan, implement, review => plan, implement, review => plan, implement, review =>........”
Chanzo: Mwandishi
Katika “spairo” hii hakuna vituo holela vya “simama nikwambie kitu.”
Badala yake, taarifa zinazopatikana katika hatua ya "planning" zinabebwa na kupelekwa kwenye hatua ya "implementation" na taarifa zinazopatikana katika hatua ya “implementation” zinabebwa na kupelekwa katika hatua ya “review” bila kusimamisha “implementation.”
Yaani, kasi ya gurudumu la “praxiological spiral” haiguswi hata siku moja.
Dr. Rose, Head of Anti-Fraud Investigation Unit, NHIF, Tanzania
V. Angalizo
Kwa ujumla, Watanzania wanataka huduma za tiba kwa kasi na viwango. Yafaa kasi ya Konokono, mizengwe na majungu yanayoigubika “service delivery cycle” niliyoijadili hapo juu vikomeshwe mara moja.
Mwisho, kumbukeni kuwa:
“When a leader fails to address the problem , then the problem becomes the leader, and the leader becomes the problem which has to be solved by subtractive elimination, additive substiution or resolution, depending on the prevailing circumstances. ”
Msisubiri kanuni hii ianze kutumika dhidi yenu.
Nawatakia tafakari njema na maamuzi ya haraka kwa faida ya wanachama wa NHIF.
VI. Orodha ya watu wanaopaswa kupatiwa nakala (distribution list)
Nakala ya dokezo hili itolewe mara moja kwa:
• Dkt. Mwenesano (Aione kwenye faili lake leo Jumapili),
• Dkt. Maganga (Aione kwenye faili lake leo Jumapili),
• Dkt. Sanga (Aione kwenye faili lake leo Jumapili), na
• Dkt. Rose (Aione kwenye faili lake leo Jumapili),
• Dkt. Lelo (Aione kwenye faili lake leo Jumapili).