Wito: Mamlaka ya Nidhamu ya Kenani Kihongosi ipeni hadhi UVCCM juu ya suala lake la ufisadi, ni doa sugu.

Wito: Mamlaka ya Nidhamu ya Kenani Kihongosi ipeni hadhi UVCCM juu ya suala lake la ufisadi, ni doa sugu.

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Kwa Sasa Kenani Kihongosi ndio kiongozi wa juu wa UVCCM kulingana na sera ya CCM ya mtu mmoja cheo kimoja kwa kuwa aliyekuwa Mwenyekiti kwa Sasa ni DC na Makamu Mwenyekiti ni waziri wa SMZ hivyo kwa nafasi yake ni Kama anahudumu kwa nafasi zote za juu za UVCCM hivyo suala la kinidhamu na kimaadili juu yake ni muhimu kwa taswira ya UVCCM.

Kipindi hiki ambacho jumuiya za CCM na CCM kinafanya chaguzi ni muhimu Sana suala la kimaadili na kinidhamu kupewa uzito wa kutosha si tu kwa viongozi wa jumuiya hizo na CCM bali kwa wanachama wote.

Kama tuhuma za Kenani Kihongosi ni za kweli basi hofu ya kupata viongozi wasio na maadili ndani ya UVCCM kwa Sasa ni kubwa na hii itapelekea UVCCM kunuka rushwa na ufisadi na kuchafuka muda mrefu.

Nani wa kusafisha uchafu huo kwa baadae? Nani atakayeamini mchakato unaosimamiwa na Kihongosi kama utatenda haki, ikiwa ishara zinaonyesha sio muadilifu?

Yote hayo yanahitaji busara na hekima zenu viongozi ili tujenge UVCCM yenye kuaminika na kuaminiwa hususani kipindi hiki cha uchaguzi ,viongozi na wanachama wa CCM wanatakiwa kuepukana na uchafu wowote.

Wito wangu kwenu mamlaka ya nidhamu na maadili ya UVCCM, suala la Kenani Kihongosi lichukuliwe hatua za haraka ili kuisafisha UVCCM na uchafu wa mtu mmoja na pia kurudisha imani kwa wenye nia za dhati za kugombea na Sasa watapata mashaka wa kupita kwao kama tu mtu mwwnye mamlaka ya mwisho ya kuwapitisha ni mla rushwa.

Pia, kiongozi fisadi na mla rushwa anatengeza taasisi ya kifisadi na inayonuka rushwa hivyo kabla Suala la Katibu mkuu wa UVCCM Kenani Kihongosi kuchafua taswira nzima ya UVCCM tunaomba hatua stahiki zichukuliwe juu yake haraka.

Ni hayo tu viongozi wangu, tunasubiri maamuzi yenu juu ya hili.
 
Back
Top Bottom