Elections 2010 Wito wa kukamatwa kwa mnajimu

Ni ujinga na upumbavu kulifumbia suala hili macho..nchi haiamini uchawi kwanini watu wanapata muda ktk vyombo vya habari kutangaza upuuzi.. Mzee wa east africa aliposema anawasiwasi mwenzao kafa wamemtia nguvuni na press conference juu tena kwa mbwembwe na kova akiwepo..sasa yeye ni nani mpaka asikamatwe tena kwa kutishia mgombea wa uraisi?
 
Huyu sheikh yahya ajiandae 'kutangulia mwalimu'. maana hata toka zamani kama mtabiri au nabii akitabiri mambo ambayo hayakutokea, huwa anakufa flat. na huyu jamaa wa majini ajiandae kutangulia...! hakuna jibu lingine kwake.
 
Huyu Shehe anabahatisha tu manake probability ya mgombea uraisi kufariki ni kubwa coz wengi wao ni wazee na wanasumbuliwa na maradhi ya moyo, hivyo anything can happen kwa mgombea kufariki kutokana na mawazo na ushindani.Sema amechemka mwaka huu manake wagombea wote wako fit na hamna kilichotokea. Pia inawezekana ni mbinu aliyopewa na CCM kuwatisha wagombea wa vyama vingine wasijitokeze kugombea kwa kuhofia kufariki. Hamna haja ya kumshtaki coz ameisha aibika mwenyewe, bora pweza Paulo alikuwa anabahatisha 100%
 
huyo ni ajenti wa shetani ivyo mwache aendelee kufanya kazi yake ,siku yako bado inakuja ndipo atakapo juta..:nono:
 
Ila ni muhimu ili liwe fundisho, maana anaweza kusema hata aliyeingia hatakaa siku mbili etc,

Fundisho pekee ni kwa yeye kuonekana muongo na huu ndiyo mwisho wake. Hakuna atakaye mwamini tena mpaka atakapo futika hapa duniani.
 
polisi wanangoja nini kukamata huyo mchawi wa nchi hii?
 
Umekosea kumwita mnajimu, ulitakiwa uweke kichwa kinasema Mchawi!. Hatuwezi kupoteza resources kwa mjinga mjinga
 
Kwanza natambua uchawi upo, ila kwa wote tunaomwamini Yehova hauna nguvu juu yetu. Na ndo mana Shekhe Yahaya kaumbuka this time, amekutana na watoto wa Yehova Nisi. Huu ni ushindi wa demokrasia na imani.
 
Jamani kuna watu wengi tuu wako mahakamani na wengine jela kwa kutishia kuua kwa maneno huyu anapaswa kuwa jela
 
Hakuna haja ya kuhangaika na watu kama hao. Njama zake tulishazishtukia huyo
 
wa mwache afe kivyake maana naskia anaumwa sana
 
Baada ya kuikomboa nchi yetu wa kwanza kukamatwa awe Chenge kwa wizi wa waziwazi ushahidi ukiwa ni kitendo cha serikali ya uingereza kuilazimisha kampuni iliyouza rada kuilipa Tz pesa ilizoiba kwa kushirikiana na fisadi CHENGE. Huyu Tapeli anatapeli wajinga wenzake asitupotee rasilimali zetu. ni wa kumdharau tu!!!
 
Utabiri wake ni wa uongo, hivyo JK atashindwa

msikatae kila kitu mnaamini kuna freemasonry na huko majuu mliko ndiko wanatawala! hesabu zilikuwa zinaonyesha jinsi wagombea walivyokamiana lazima mmoja atadondoka...! tushukuru lakini lolote laweza likatokea wakati wowote...! kila mtu kwa dini yake asali kuiombea amani na utulivu nchi yetu..na kwa mwaka huu wapinzani watafanya vizuri lakini...kubwa tukubali matokeo...! Hongera Wagombea wa vyama vyote tusubiri uamuzi wa Watanzania... na heshimu uamuzi wao wajumla lakini wa mtu binafsi sawa jamani..!
 
Unamwongelea yule mnajimu wa thithiemu? Me nadhani anyongwe tu!
 
Sijui watajificha wapi na JK wake. Hapa Kikwete anapaswa aelewe kuwa huyo mnajimu wake huwa anamdanganya na ndo maana wananchi wamemchoka, hawamtaki.
 
Jamani kuna watu wengi tuu wako mahakamani na wengine jela kwa kutishia kuua kwa maneno huyu anapaswa kuwa jela
sure, sijui kwanini mpaka sasa bado yupo mitaani. Hivi ameenda kupiga kura?
 
Sijui watajificha wapi na JK wake. Hapa Kikwete anapaswa aelewe kuwa huyo mnajimu wake huwa anamdanganya na ndo maana wananchi wamemchoka, hawamtaki.

Hata huo ulinzi aliokuwa anamwahidi nao ni feki, sasa mkwere inabidi afungue macho huyu mzee ameshamchakachua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…