Wito: Waziri Jafo tumeona maelekezo ya Geita na Mpanda ni maamuzi mazuri, Temeke je?

Wito: Waziri Jafo tumeona maelekezo ya Geita na Mpanda ni maamuzi mazuri, Temeke je?

alexander paulo

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
492
Reaction score
155
Kupitia vyombo vya habari kwa siku za hivi karibuni tumeona Mh Jafo akimsimamisha Mkurugenzi wa Geita kupisha uchunguzi na pia ametoa maelekezo kama hayo kwa Halmashauri ya Mpanda.

Lakini Mh. Jafo watu wengi wanajiuliza kuna lile Gari la Mkurugenzi wa Temeke ambalo limenunuliwa 400M mwaka 2019 na pia inasemekana kanunua magari aina ya Tata ya kubebea watumishi ambayo nayo wanadai ni mabovu tunaiwekaje hii? Mh chukua hatua kali Mh Raisi anakuamini sana.
 
Kwa ujumla TAMISEMI kumeoza, Morogoro barabara mpya tu ni mashimo kwa kwenda mbele. Hata soko jipya halifanani na thamani ya fedha iliyotumika kulijenga. Jafo inabidi akaze buti ili atoboe 5yrs.
 
Mm huwa sina Imani na jafo na makatibu wake wakuu wote wale wa3 kwanza ni wizara inayoongoza kwa kupokea rushwa na kufanya madudu.Hii wizara inahitaji mtu creative kama january Makamba.
 
Jafo sinawahi kumuamini zaidi anabebwabebwa tu, yeye yake ni kutembea na kamera na kutishatisha wakuu wa Idara ila hana vision wala mission ya ku accomplish kabisa, kwanza hajiamini na bahati mbaya Mwazir ama nisema viongozi wengi wanaona kufokafoka ndio uongozi
 
Huo ni uozo wetu watanzania. Badala ya kumnyooshea kidole Jafo tungeanza kujinyooshea kidole sisi wenyewe. Jafo, au hata kiongozi mwingine yeyote, wanapambana na uozo wetu sisi wenyewe, sisi hawa hawa (watanzania), siyo aliens, ndio tunasababisha mauozo hayo yote. Pamoja na kuwatupia lawama watendaji wetu, nadhani ni vyema tufike mahali tuanze kijinyooshea vidole sisi wenyewe.
 
Kwa hali hii kuna haja sasa ya kupitia matuizi ya hawa wakurugenzi wetu. Mimi huwa najiuliza vipaumbele vya baadhi ya wakurugenzi nini ikiwa mkurugenzi yupo halafu wanafunzi katika halmashauri yake hawana madawati au wanaupungufu wa matundu ya vyoo, au vyumba vya madarasa ni vichache.

Hakuna kitu kibaya kama kuwa na viongozi ambao hawana maono watu ambao hawana picha nzuri ndani ya ubongo wao kuhusu nini kinapaswa kuwa ndani ya miaka kadhaa.

Kwa bahati mbaya jamii yetu huwa inawabeza na kuwapiga majungu watu wenye maono na wenye kuona mbali ili kuwakwamisha mfano mzuri ni Makonda.
 
Huyu DED madiwani wa manispaa ya Temeke wanalalamikia kutumia ubabe kwa walimshutumu kununua magari ya kifahari ya pesa nyingi kwa kutumia ubabe bila kuwashirikisha sawa. Kama haya yana ukweli na hajatumbuliwa hadi sasa, nani anamkingia kifua?
Rais wetu mpendwa JPM tupia jicho lako kali mahali hapa.
 
Huyo achana nae. Ni mungu mtu kwa sasa pale Tmk na DSM nzima. Makonda no2
 
Hii tunaita baada ya fisi kula mbuzi na kondoo kuisha sasa wameanza kulana wao kwa wao.
 
Huyu DED madiwani wa manispaa ya Temeke wanalalamikia kutumia ubabe kwa walimshutumu kununua magari ya kifahari ya pesa nyingi kwa kutumia ubabe bila kuwashirikisha sawa. Kama haya yana ukweli na hajatumbuliwa hadi sasa, nani anamkingia kifua?
Rais wetu mpendwa JPM tupia jicho lako kali mahali hapa.
Hao madiwani wanajilinda. DED anawezaje kuwalazimisha? Kama ni hivyo basi hawastahili nafasi walizokuwa nazo. Walikuwa na mamlaka ya kukataa na asingewafanya kitu.

Amandla...
 
Kupitia vyombo vya habari kwa siku za hivi karibuni tumeona Mh Jafo akimsimamisha Mkurugenzi wa Geita kupisha uchunguzi na pia ametoa maelekezo kama hayo kwa Halmashauri ya Mpanda...
Yaani sasa naamini wapinzani walichelewesha maendeleo ya Watanzania. Kumbe haya yote ni wapinzani walikuwa wana sababisha.. Kweli Ccm imeoza. Tuombe Mungu tutoke hapa..
 
Jafo sinawahi kumuamini zaidi anabebwabebwa tu, yeye yake ni kutembea na kamera na kutishatisha wakuu wa Idara ila hana vision wala mission ya ku accomplish kabisa, kwanza hajiamini na bahati mbaya Mwazir ama nisema viongozi wengi wanaona kufokafoka ndio uongozi
Exactly
 
Back
Top Bottom