wivu unasababishwa na nn katika mapenzi?

twenty2

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Posts
296
Reaction score
32
kwa mtazamo wangu wivu unasababishwa na upendo wa kweli na wa dhati uliokuwa nao kwa mpz wako.
 
bila ya wivu hakuna mapenzi,, lazima kama unapenda utakua na wivu, na hiyo ina kuja wenyewe tu,
 
Wivu ni udhaifu wa kijinga sana,hakuna mahusiano yoyote kati ya wivu na mapenzi ya kweli,wivu ni ujinga walionao wasiojiamini katika mahusiano!
 
kuna wengine hata hawana mapenzi ya kweli ila wana wivu,mfano umeachana na x wako na ana mtu wake na wewe una wako but unakuta anakuonea wivu akikuona na mwingine.
Kuna wivu unaotokana na tamaa za mtu.
 
Wivu ni udhaifu wa kijinga sana,hakuna mahusiano yoyote kati ya wivu na mapenzi ya kweli,wivu ni ujinga walionao wasiojiamini katika mahusiano!

mapenzi ya kweli wivu ni lazima japo usipite kipimo kwa kiasi
 
Wivu ni sehemu ya nature ya binadamu (wote wanawake kwa wanaume), uwe na mapenzi ya kweli au hata kama unazuga tu. Pia ni sehemu ya nature kwa viumbe wengine wa kiume. We mwangalie jogoo asivyotaka jogoo mwingine amwingilie ktk mitetea yake, pia angalia mbuzi beberu ndo utajua wivi ni asilia. Anayeonekana hana wivu kwenye mauhusiano ni kuzuga tu, tena ni kwamba anajitahidi tu kuficho asiuonyeshe ila moyoni mwake wivu umejaa tele!!
 
mapenzi ya kweli wivu ni lazima japo usipite kipimo kwa kiasi
Usidanganywe,hakuna kitu kama hicho,wivu ni matokeo ya kutokujiamini,kama unajiamini na unamuamini mtu wako wivu wa nini?
 
kwa mtazamo wangu wivu unasababishwa na upendo wa kweli na wa dhati uliokuwa nao kwa mpz wako.
Wivu ni ishara ya mapenzi - ukiona mpenzi wako hakuonei wivu ujue anachakachuliwa na wengine vya kutosha na wewe anakuona takataka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…