Wivu Unawatafuna Sana Watanzania

Wivu Unawatafuna Sana Watanzania

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Watanzania sijui tuna shida gani jamani, labda ni umaskini unasumbua sana ila ukweli hatupo sawa. Imagine mtu anaonea wivu ndoto ya mtu!

Waswahili wanasema akumulikie mchana usiku atakumaliza.

Juzi kati Diamond alisema ana ndoto ya kuwa Tajiri no. 1 duniani. Elewa nini maana ya ndoto ya kutaka. Ndoto sio deni hata usipotimiza ila watu, walimpinga sana. Hivi sisi hatuna ndoto? Dah kama hauna ndoto katika maisha yako aisee we sio binadamu ni vampire. Watu wanasherekea mwaka mpya na kuweka malengo angalau ndani ya mwaka huu nifanye hichi nifike hapa.

Binafsi mwaka huu nilikuwa na ndoto ya kulima kilimo cha umwagiliaji hadi sasa nipo shambani napambana nimeacha kitanda.

Tisa kumi kuna watu humu wanaonea wivu hadi thread za watu. Kuna mtu ukiposti kitu akiona watu wanachangia anakuja tu kuleta shida kwenye hiyo thread. Nilichogundua ni wivu tu unawasumbua hamna kitu kingine unakuta thread ni ya msingi ina funzo zuri sana kwa jamii ila mtu anakuja kuharibu tu for no reason.


Mtu anaonea wivu ata wazo tu la mtu. Kuna jamaa waliua mbwa wa jirani yangu German shephard kisa jamaa alikuwa anatembea, anafanya nae mazoezi jamaa wakasema anawatambishia mbwa na kweli wakampeleka mbele za haki.

Tuache wivu usio na msingi. Lazima tukubali katika maisha tumetofautiana kuanzia sura, akili, hekima, busara, maumbile, elimu, kipato n.k! Na aliyepewa kapewa tu hata ufanyaje Mungu atampa tu. Hatuwezi kuwa sawa hata siku Moja.

Angalia Waarabu Mungu alimwambia Abrahamu msikilize mke wako sababu hata mtoto wa mjakazi wako ntamfanya taifa.

Cha ajabu kila anapokaa Mwarabu chini kuna mafuta anachimba tu. Wale hata tukiwaleta Manzese wanaweza chimba mafuta ya kutosha. Sisi tumepewa Madini hata kuchimba tunashindwa.

Tubadilike tuache wivu usio na msingi.
 
Ni umasikini tu mamaeh, hakuna sababu ingine..matajiri wanatoa wap muda huo
Ni mamamaskini haya mahusda na mijichawi
 
Back
Top Bottom