Wivu wasababisha azinyofoe Nyeti za Mpenzi wake

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Wivu wasababisha azinyofoe Nyeti za Mpenzi wake

Madaktari walifanikiwa kuziokoa nyeti za MbelgijiMonday, May 18, 2009 4:22 PM
Mwanamke mmoja wa nchini Thailand amezing'ata na kuziacha zikining'inia nyeti za mpenzi wake raia wa Ubelgiji baada ya kugundua alikuwa na kimada nje.Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Thailand, mwanamke huyo alizingata nyeti za mpenzi wake raia wa Ubelgiji kiasi cha kuaziacha zikiwa zinaning'inia.

Kwa bahati nzuri madaktari walifanikiwa kuziokoa nyeti hizo na kuzishonea tena sehemu yake.

Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 56 anapatiwa matibabu hospitali akiugulia majeraha makubwa aliyoyapata kwenye uume wake kufuatia tukio hilo lililotokea jana kwenye pwani ya mji wa utalii wa Pattaya.

"Hadi sasa hatujui jina la mtuhumiwa au kama anafikiria kumpandisha kizimbani au la" alisema msemaji wa polisi wa Pattaya.

"Aling'atwa na kujeruhiwa vibaya sana uume wake, lakini hakuunyofoa kabisa aliuacha ukining'inia" alisema msemaji huyo wa polisi.

Vyombo vya habari vya Thailand viliripoti kwamba wapenzi hao walikuwa kwenye mgogoro mkubwa baada ya mwanamke huyo kugundua kuwa Mbelgiji huyo alikuwa akitoka kimapenzi na mwanamke mwingine raia wa Thailand.

Wasemaji wa Hospitali ya Pattaya walisema kwamba Mbelgiji huyo alikuwa hataki kuliongelea suala hilo kwa waandishi wa habari na alikataa kuelezea jinsi ilivyokuwa.
 
Mods Nadhani hii imekosea njia Ipelekwe kwake
 
habari hii ina mahali pake iwashe huko itaeleweka zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…