Wivu wetu uko kwenye kitu gani hasa?

Wivu ni udhaifu halafu ni hisia hasi,haujawahi kuleta matokeo chanya wakati au mahali popote!
 
PetCash hauja muelewa mtoa hoja. Mwenzio anazungumzia wivu katika mapenzi wakati wewe unazungumzia wivu katika masuala ya maendeleo. Msome vizuri.
 
wivu katika mapenzi ni muhimu jaman...hata kama ni kwa asilimia 1,but kama unampenda kwa dhat mwandan wako..aaaah,kawivu lazima katakuwepo.
 
wivu katika mapenzi ni muhimu jaman...hata kama ni kwa asilimia 1,but kama unampenda kwa dhat mwandan wako..aaaah,kawivu lazima katakuwepo.

Hebu niambie wivu maana yake nini na nini umuhimu wake!
 
Ukipenda daima utajenga dhana fulani ya umilikishi yaani kujenga mawazo ya kana kwamba yule mtu ni wa kwako tu..na haupo tayari kumwona akiwa karibu na mwingine! Wivu upo katika many aspects, si kwa wapenzi tu hata marafiki..
 
Hapo kwenye bold, tunachoonea wivu ni ile haki yangu ya penzi juu ya yule nimpendae hususan kama kuna dalili ya kuitoa haki hiyo kwa mtu asiye mhusika!!!
 
PetCash hauja muelewa mtoa hoja. Mwenzio anazungumzia wivu katika mapenzi wakati wewe unazungumzia wivu katika masuala ya maendeleo. Msome vizuri.
Litty asante, Ila kuwa na a great love life ni maendeleo. Sema tu mimi nimeamua kuwa general.
 
Last edited by a moderator:
Wivu muhimu kwa umpendae hasa pale unapohisi kuna mtu anakuibia usingizi unakosa....
 
Hapo kwenye bold, tunachoonea wivu ni ile haki yangu ya penzi juu ya yule nimpendae hususan kama kuna dalili ya kuitoa haki hiyo kwa mtu asiye mhusika!!!

Unajuwa HP, kinachonishangaza mimi kuwa kuna wengi wenye wivu kwa watu wao iwe mke au mume lakini huwa wanakwenda kwa watu wengine ambao inawezekana wao wenyewe wanakiri kuwa watu wao wana vitu vizuri zaidi kuliko wanavyovifatia nje. Kibaya ukiwauliza wanakwambia wanawapenda watu wao na inawezekana wanawapenda kweli.
 
Wivu ni udhaifu halafu ni hisia hasi,haujawahi kuleta matokeo chanya wakati au mahali popote!

Mimi siamini kuwa wivu ni udhaifu bali ni njia moja ya kujali chako, of course kila kitu kikienda extreme ni kibaya!
 
wivu katika mapenzi ni muhimu jaman...hata kama ni kwa asilimia 1,but kama unampenda kwa dhat mwandan wako..aaaah,kawivu lazima katakuwepo.

Katika mapenzi huwa tunashare mahusiano yetu na wanaotuzunguka, sasa huku kushare tunashare mpaka wapi na kuanzia wapi wivu (Hisia ya kukimiliki peke yako) unaanzia?
 
Ukipenda daima utajenga dhana fulani ya umilikishi yaani kujenga mawazo ya kana kwamba yule mtu ni wa kwako tu..na haupo tayari kumwona akiwa karibu na mwingine! Wivu upo katika many aspects, si kwa wapenzi tu hata marafiki..

Kwa upande wako Da Amina umiliki wako peke yako kwa shemeji unaanzia wapi? Nasema hivyo kwani shemeji ana watu wanamzunguka ambao atawapa sehemu mahusiano yake.
 
Kiongozi ukiona hivyo, ujue ni suala la tamaa za mwili linakuwa limechukua nafasi yake. Unakuta mtu ana mke anayempenda, akapita mtu mwingine mwenye figure ya kuvutia akashikwa na tamaa akamtokea na kutembea naye wakati moyoni mwake hampendi, anafanya hivyo kukidhi mahitaji ya mwili kwa wakati huo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…