Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Mwanamuziki wa miondoko ya hip-hop nchini marekani maarufu kwa jina la Wiz Khalifa, amethibitisha kupitia ukurusa wake wa twitter kuwa amepata maambukizi ya virusi vya corona. Amewatoa wasiwasi mashabiki wake kwa kusema hana dalili zozote, ila anawaomba wakae mbali naye kwa muda kidogo. Mwanamziki huyo alikutana na msanii Diamond Platnumz wiki mbili zilizopita hatua iliyoashiria uwezekano wa kutoa wimbo pamoja.