Wizara ya afya kuweni makini

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Posts
17,057
Reaction score
7,611
Nchi jirani wetu wote wana matatizo na ni threats kwa afya za watu wetu.

Kuna Congo, Burundi na Uganda zote hizi haipiti muda utasikia magonjwa yamezuka na ndo hapo tunapoanza kuhaa na kuzuia na matibabu. Kibaya kuliko vyote katika mikoa inayopakana na nchi hizi hakuna vituo maalum na vya kisasa ambavyo viko tayari kwa ajiri ya kudili na milipuko hii ya haraka.

Chukulia mfano katika mkoa wa Kagera, hospitali ya mkoa iko 90km kutoka mpakani mwa Uganda. Fikilia linapokuwa limetokea hili na ushaanza kupata wahanga utatumia mda gani kuwasafirisha hadi wakafike mkoani, na kwanini iwe hivyo? Ni kwanini pale pale mpakani kisijengwe kituo/unit maalum kwa ajiri ya kutackle uingiaji wa magonjwa haya ambayo yamekuwa too repetitive na periodical?

Kama mlivyoweka vituo vya one stop centre, nilitegemea hivyo hivyo ingefanyika kwa magonjwa haya. Leo utasikia kimeta, kesho tena mtasikia ebora, na mengine kibao. Ni kwanini hadi tusubiri yatokee wakati tupo tunaona na tunasikia?

Msisahau ugonjwa wa Ukimwi ulitokea kwa majirani zetu Uganda, kwanini tusubiri yaje mengine as if bado tunaishi katika zama zile za kutofahamu? Mikoa yote hii Kigoma, Katavi, Rukwa n.k, yote haiko salama, kama kweli mnajari maisha ya watanzania inakuwaje mnashindwa kuona umuhimu wa kuchukua hatua hizi kuliko kusubiri hadi litokee. Tufanye mambo kisomi na tuchukue hatua mapema kabla hari haijatubadilikia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…