DOKEZO Wizara ya Afya, mamlaka za kiusalama chunguzeni kwa kustukiza hospitali ya Lupa iliyopo wilayani Bunda

DOKEZO Wizara ya Afya, mamlaka za kiusalama chunguzeni kwa kustukiza hospitali ya Lupa iliyopo wilayani Bunda

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2023
Posts
445
Reaction score
1,094
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano. Kuna malalamiko yameripotiwa kwa siku za karibuni kuhusu hospitali ya LUPA iliyopo ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda.

Malalamiko ni mengi ila nitajikita kwa mgonjwa x (jina linahifadhiwa kwa Sasa). Huyu dada alifika hapo kutibiwa baada ya kubaini ana dalili za ugonjwa wa maralia.

Akiwa hapo hospitali aliomba apatiwe dawa za mseto ila cha kushangaza mhudumu alionyesha kutokubaliana na mgonjwa huku naye akimlazimisha mgonjwa atumie aina ya dawa zilizoonekana kuwa mpya kwa mgonjwa.

Kwa shingo upande mgonjwa akazitumia! Wiki moja baadae hali ya mgonjwa husika ikabadilika sana kitendo kilichopelekea ndugu zake kumpeleka kwenye moja ya hospitali za rufaa iliyo Mwanza.

Baada ya kuulizwa historia yake alieleza kila kitu kuanzia kupimwa na kukutwa na maralia mpaka kupewa tiba. Cha kushangaza alipopimwa kwa mara nyingine akabainika kuwa na vijidudu vya maralia! Pamoja na hayo mgonjwa pia alikuwa na tatizo jingine ambapo alitibiwa kwa kuchomwa sindano.

Hili nalo ilionyesha dawa zilizotumika zilikuwa zimekwishamaliza muda wake.Yaani matatizo yote mawili maralia na Hilo jingine alitibiwa kwa dawa zilizokwishamaliza muda wake!

Kwa kuongezea madaktari wakamueleza ulikuwa almanusra tu apooze mawili wake endapo sindano zingechomwa kwenye baadhi ya maeneo ya mwili wake(Hili nimeshindwa kulielezea kitaaluma)

Wito wangu mamlaka husika fanyeni msako wa KUSTUKIZA hospitalini hapo mfanye ukaguzi wa nguvu.Lakini pia hili lisiishie hapo bunda tu bali lifanywe nchi mzima.Kufanya hivi kutaokoa maisha ya wananchi wengi.
Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom