Wizara ya Afya: Mmepeleka wapi pesa za kujikimu madaktari bingwa wanafunzi

Wizara ya Afya: Mmepeleka wapi pesa za kujikimu madaktari bingwa wanafunzi

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Nikiwa kama mwanafunzi wa udaktari bingwa ninashangazwa sana jinsi wizara ya afya inavyochelewesha malipo kwa wanafunzi wa udaktari wanaosomea digrii ya pili. Imekuwa ni kawaida sana malipo ya wanafunzi kucheleweshwa sana pasipo sababu zinazoeleweka. Ni ajabu kwamba tumeshaanza mwaka mpya wa masomo lakini pesa za mwaka wa jana mpaka sasa hatujalipwa. Karibu kila mwanafunzi anayedhaminiwa na wizara ya afya anadai takribani milioni moja na laki 8. Nasikia wenzetu Muhimbili Chuo kila mmoja kawekewa laki tatu kupunguza deni hilo la mwaka wa masomo uliopita. Ajabu ukienda wizara ya afya hakuna mtu anayejali. Tukidai haki tunapigwa virungu. Sehemu ndogo ya pesa za mwaka huu wa masomo yamkini zitatoka mwezi february mwakani, wakati vyuo vimefunguliwa toka septemba mwishoni.
Watu tunajiuliza hivi hii serikali kupitia wizara inazipeleka wapi pesa hizi? Hivi kuna priorities ngapi ambazo wizara husika yatakiwa izifanyie kazi kama si hizi?
Tunatamani mheshimiwa RAIS ajue lakini bahati mbaya yanaishia vinywani mwetu.
Yaani sisi miafrika shida tupu.
 
rais gan,hata akilifahamu hawez fanya jambo lolote b'se afya ya watanzania(ambao si familia yake) si kipaumbele kwake
 
Wewe dawa tu hazipo sasa unatuambia nyie mnaosoma tena degree ya pili. Msituchoshe ngoja tutafute hela ya MSD nyie hata masomo yaki ahilishwa hiyo degree ya kwanza itakuwa na manufaa makubwa tu. Haa haa haa this country is veri puwa
 
"Sasa hivi tumejikita katika katiba mpya,uandikishaji upya wa wapiga kura na Uchaguzi,huko ndiko tunakoelekeza mabilioni ya walipa kodi wa nchi hii lakini mambo ya kimaendeleo kama haya hayatuhusu.Sasa hivi pia tunajenga na kuimarisha chama na matumbo yetu.Watanzania watajua wenyewe na ole wako ulete chokochoko za kugoma na maandamano,nguvu ya dola imejipanga kikamilifu"
Kweli hii ndo Tanzania nchi ya neema kwa baadhi ya walionacho huku asilimia kubwa ambao ni walala hoi wakiachwa njia panda kana kwamba hawastahili kupata haki zao,mbaya zaidi sasa tunauawa kimya kimya kwa kunyimwa hata dawa katika hospitali za uma kutokana na deni dogo inalodaiwa serikali,(nimesema dogo ukilinganisha na hela nyingi tunazosikia kila kukicha zinatafunwa na wachache.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...!!!!!!
 
Dogo achana na udaktari... Tanzania Siasa inalipa sana!!!!!
 
Siasa inalipa mkuu. Watoto wakiugua unapeka utakako. Kagombee hata udiwani.
 
Back
Top Bottom