tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Nikiwa kama mwanafunzi wa udaktari bingwa ninashangazwa sana jinsi wizara ya afya inavyochelewesha malipo kwa wanafunzi wa udaktari wanaosomea digrii ya pili. Imekuwa ni kawaida sana malipo ya wanafunzi kucheleweshwa sana pasipo sababu zinazoeleweka. Ni ajabu kwamba tumeshaanza mwaka mpya wa masomo lakini pesa za mwaka wa jana mpaka sasa hatujalipwa. Karibu kila mwanafunzi anayedhaminiwa na wizara ya afya anadai takribani milioni moja na laki 8. Nasikia wenzetu Muhimbili Chuo kila mmoja kawekewa laki tatu kupunguza deni hilo la mwaka wa masomo uliopita. Ajabu ukienda wizara ya afya hakuna mtu anayejali. Tukidai haki tunapigwa virungu. Sehemu ndogo ya pesa za mwaka huu wa masomo yamkini zitatoka mwezi february mwakani, wakati vyuo vimefunguliwa toka septemba mwishoni.
Watu tunajiuliza hivi hii serikali kupitia wizara inazipeleka wapi pesa hizi? Hivi kuna priorities ngapi ambazo wizara husika yatakiwa izifanyie kazi kama si hizi?
Tunatamani mheshimiwa RAIS ajue lakini bahati mbaya yanaishia vinywani mwetu.
Yaani sisi miafrika shida tupu.